Social Icons

Monday, August 8, 2011

TATIZO LA MAFUTA LAZIDI KUTIKISA NCHI

Mmoja wa wateja wa mafuta akiburuzwa na askari polisi waliyokuwa wametanda kwenye kituo cha mafuta cha Big Born, baada ya kukosea masharti ya foleni iliyokuwepo hapo na kupenya kwa mbele zaidi kwaajili ya kupata huduma hiyo.
Raia hyo akisongeshwa kwenye Defender, tayari kwa mapumziko ya kijeshi zaidi.
t... akisaidiwa kupanda karandinga.
... alisukumizwa namna hiyo.
Mmoja wa wateja wa mafuta hayo akisepa na kidumu cha mafuta baada ya kupatiwa huduma.
Afande akielekeza magari namna ya kupanga katika foleni hiyo
Jamaa akikokota gari tayari kwa kusogeza kupata huduma hiyo.
Afande na 'mtutu' wake akikagua usalama wa kituo hicho.
Wengine na vigereni mkononi tayari kwa kunusuru tatizo hilo
Mambo ....
Baadhi yao wakipatiwa huduma.
Njemba akisukuma gari hilo tayari kwa kupata huduma.
Baadhi ya magari yakiwa kwenye msululu wa kuelekea kupata huduma ya mafuta.
Madreva wa bajaj wakijadili namna ya kupata mafuta mapema ili waendelee na kazi yao ya kuchukua abiria, kandokando ya kituo cha mafuta hicho.

TATIZO la Ukosefu wa Nishati ya Mafuta wazidi kuitesa nchi kutokana na kuwa adimu, ambapo baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wanadaiwa kuitisha mgomo baridi, kwa kisingizio ya nishati hiyo kutopatika kwenye visima vya mafuta wanakochukulia.

Mateja20, jioni hii ilipita mitaa ya Sinza Mori katika kituo cha Big Born na kukuta kasheshe la aina yake ambapo Askari polisi wakiwa wamemkwida muungwana mmoja baada ya kuvuka foleni na kusonga kwa mbele zaidi akitaka kumiminiwa mafuta kwenye releni yake ili awahi usafiri wake uliyokuwa umemzimikia, barabarani na juhudi zake hizo kuishia mikononi mwa maafande waliyokuwa wametanda kwenye kituo hicho kwaajili ya usalama, na kuelekeza foleni ya magari yaliyokuwa yakielekea kituoni hapo tayari kwa kupata mafuta ambayo pia yalikuwa yakitolewa kwa sharti la kutozidisha lita 20.

Pamoja na hilo katika kituo hicho kulikuwa na mafuta aina ya Petrol tu huku Diesel ikiendelea kuwa tatizo kubwa pande hizo ambapo magari yaliyohitaji huduma hiyo yaliishia kupanga foleni.

0 comments: