Social Icons

Thursday, August 11, 2011

M/KITI WA (WAMA ) MAMA SALMA KIKWETE AWASIHI WAZAZI NA WALEZI

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA ) Mama Salma Kikwete akisoma nakala ya RAPID WOMEN Model ambayo ni kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke, matumizi ya kielelezo hicho yanalenga zaidi wanawake viongozi katika kuhamasisha jamii. Muundo huo wa kitendea kazi uliwasilishwa na Dr. Sara Clark (hayupo pichani) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International leo katika ofisi za WAMA zilizopo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) (katikati) Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dr. Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International na Millicent Obayo ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa kampuni hiyo wakati walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwasilisha muundo wa kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke.
Dr. Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya Futures Group International akimuonyesha Mke wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA ) Mama Salma Kikwete (kulia) nakala ya RAPID WOMEN Model ambayo ni kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke, matumizi ya kielelezo hicho yanalenga zaidi wanawake viongozi katika kuhamasisha jamii.

0 comments: