Social Icons

Tuesday, August 9, 2011

KONDOO MWENYE MAAJABU AZIDI KUSHANGAZA RAIA

KUZALIWA kwa kondoo mwenye maneno ya kiarabu katika kijiji cha Uduru Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kumefanya kijiji kupata wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali kufika kushuhudia tukio hilo na hasa waumini wa dini ya Kiislamu.

Kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita aliyekuwa na neno la kiarabuupande wa kulia ubavuni mwake lenye maana ya neno ya YASINI kwa tafrisi ya Kiswahili alisababisha waumini wa madhehebu, ya Kiislamu kumimika kijijini hapo kushuhudia tukio hilo
Kondoo huyo amezaliwa katika familia ya waumini wa dini ya Kikristo.

Amevuta hisia za waumini wengi hasa wakazi wa kijiji hicho, kushudia tukio hilo la ajabu na la na ambalo halijawahi nkutokea katika nchi hii familiahiyo,

Akizungumzia tukio hilo kijiji hapo mmiliki wa Kondoo huyo, Grace Eliumini Massawe (55) alisema kwamba, kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kuwa alikuwa na neno hilo ubavuni mwake kutokana na mama wa mbuzi huyo, kumficha ndani kwa wiki hizo zote bila kutoka nje.

Aidha alisema kuwa baada ya kuzaliwa kondoo huyo dume, mama yake alibadilisha tabia kwani awali alikuwa akila na wenzake jambo ambalo sasa ni kinyume kwani baada ya kuzaa kwa kondoo huyo hafanya hivyo.

Mmiliki wa kondoo huyo aligundua kundoo wake ana neno la kiarabu baada ya kutolewa nje na mama yake ambapo alifikiri kuwa ilikuwa ni herufi ‘W’ yenye rangi ya dhahabu iliyofifia .

“Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi hali iliyopelekea kutafuta msaada ili kuweza kulitambua maana yake halisi kutoka kwa waumini wa dini ya kiislamu,

“Mara baada ya kufika waumini mbalimbali wa thehebu la Kiislamu nyumbani kwangu waligundua kuwa kondoo huyo dume alikuwa ameandikwa kwa kiarabu neno lenye tafrisi ya Aya ya ‘YASINI' ,
“Pia waumini hao walinieleza neno hilo ni muhimu sana katika kitabu kitakatifu cha quran, na kwamba ni kitovu cha kitabu hicho na pia ni moja ya sura muhimu sana ndani ya kitabu hicho kitakatifu". alisema kwa kusisitiza mama huyo.

Katibu wa Baraza la Waislamu mkoa wa Kilimanjaro BAKWATA Sheikh Rashid Mallya, alikiri kufika kumshuhudia kondoo huyo, nakueleza kuwa maandishi yanayosomeka ubavuni mwa kondoo huyo ni sahihi kama yanavyosomeka katika kitatu kitakatifu cha quran.

Sheikh Mallya alisema aya ya maandishi hayo katika kitabu cha quran ni moja ya sura inayoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake.

Sheikh Mallya, aliongeza kufuatia maneno hayo, hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya kiislamu, kuwa watakatifu zaidi hasa siku hizi za mfungo wa mwezi mtukufu.



0 comments: