Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka nchini China, Zhao Shaohua, akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinga (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo.
Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Picha zote na Anna Nkinda-MAELEZO Waziri Mkuu,Mizengo Pinga, akiangalia zawadi ya chombo cha kuwekea sukari alichopewa na Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (kulia) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo. Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Anjela Ngovi, akimvalisha kanga Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia . Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Picha zote na Anna Nkinda-MAELEZO
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
0 comments:
Post a Comment