Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana na Fabio wa Man U |
Friday, July 29, 2011
MRISHO NGASA AFUZU MAJARIBIO YA KUKIPIGA MAREKANI
MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam, Mrisho Ngasa, amefuzu majaribio yake ya kuichezea timu ya Seattle Sounders ya Marekani inayoshiriki Ligin Kuu ya England.
Ngasa aliondoka jijini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kufanya majaribio na timu hiyo iliyofika dau la kumnyakua kwa ajili ya kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Aidha baada ya kuwasili nchini Marekani Ngasa alifanyiwa majaribio ya kwanza katika mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Manchester United ya Englandm, ambapo Ngasa alichezeshwa dakika 15 za mchezo huo na kuwaacha hoi mashabiki lukuki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Pamoja na jitihada za Ngasa alizoweza kuonyesha katika dadkika hizo 15 na kukosa bao katika dakika za mwisho za mchezo huo, lakini timu yake ilibugizwa mabao 7-0.
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment