Social Icons

Tuesday, July 26, 2011

MNENGUAJI WA TWANGA PEPETA AFANYIWA KITCHEN PARTY

Baadhi ya Wanenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwa kwenye Kitchen Party ya mnenguaji mwenzao, Betty Jonson Mwangosi 'Baby Tall' iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, tayari kwa maandalizi ya ndoa yao ambayo itafungwa Julai 27 mwaka huu nyumbani kwao na Baby Tall, Popobawa, jijini Dar es Salaam.

Mama mzazi wa Baby Tall (aliyenyoosha mikono mbele), akiingia ukumbini hapo.

Kiongozi wa bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta', Luiza Mbutu (aliyetega mgongo), akicheza kiduku ukumbini hapo.

Bibi harusi mtarajiwa Baby Tall (kushoto), akizama ukumbini hapo na mpambe wake kulia.

Mmoja wa wazazi wake na Baby Tall, akinengua kwa furaha ukumbini hapo.

Baby Tall, akiwa kwenye pozi mbele ya meza kuu muda mfupi baada ya kuingia ukumbini hapo.

Mshereheshaji wa Party hiyo, Maimartha Jesse (kushoto), akimkaribisha Luiza Mbutu aongee jambo kwa bibi harusi mtarajiwa.

Luiza akitoa usia kwa Baby Tall.

Mwimbaji wa Bendi ya African Stars international Khadija Mnoga (kushoto), akiwa kwenye pozi na Mnenguaji wa Mapacha Watatu, Saburina Mbetembete.

Sabrina Mbetembete, akiwa kwenye pozi na mmoja wa wanenguaji wa Bendi ya African Stars International Vick

Muimbaji wa Twanga Pepeta Janeth Isinika akifungua 'Shampeni' ukumbini hapo.

Janeth, akimimina Shampeni hiyo kwa baadhi ya wageni waarikwa.

Luiza Mbutu (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.

Kimwana Twanga Pepeta namba mbili 2007, Husna Iddi 'Sajenti' akiwa kwenye pozi Ukumbini hapo.

Baby Tall, akikabidhiwa mic tayari kwa kutambulisha ndugu zake kwa wageni waarikwa.

Baby Tall, kabla ya kuanza kutambulisha, alikosa neno na kubaki akijing'ata ng'ata.

Baby Tall, akimtambulisha mama yake mzazi

Mama mazazi wa Baby Tall, akisikiliza ujumbe kutoka kwa mwanaye.

Baby Tall, akiwatambulisha dada zake kwenye meza hiyo.


Luiza Mbutu, akiongea jambo na Baby Tall, amara baada ya kumtambulisha kama dada yake ukumbini hapo.
Posted by Picasa

0 comments: