MTANGAZAJI wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, kinachorushwa hewani kupitia kituo cha Times FM, Khadija Shaib ‘Dida wa G’, juzikati , alisheherekea harusi ya kuolewa kwake, na mwanamume mwingine aitwaye Gervas Mbwiga, ambapo watu walifurahi na kuburudika vilivyo, Risasi Mchanganyiko lina data kamili.
Sherehe za haruri hiyo zilizoshuhudiwa hatua kwa hatua na paparazzi wetu, hizo zilifanyika Julai 17 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa New Msasani Club jijini Dar es Salaam, na kuhudhuliwa na watu kibao kutoka pande mbalimbali za jiji.
Yaliyojitokeza kwenye sherehe hiyo ni pamoja na na ukumbi huo kuwa na joto la kukithili, ingawa dakika chache kabla ya shughuli hiyo kumalizika, umeme ulirudi na kuwashwa viyoyozi ukumbini hapo.
Katika burudani, sherehe hiyo ilitawaliwa na bendi za mwambao, ambapo kundi zima la Mashauzi Clasic Bendi, lilitumbuiza chini ya mmiliki wake Aisha Ramadhani 'Isha mashauzi', huku Mzee yusufu naye akikonga nyoyo za wageni waarikwa kwa niaba ya kundi lake la Jahaz Modern Taarab.
Chakushangaza zaidi kwenye hafla hiyo, ni kukosekana kwa mastaa wa filamu kama ilivyotalajiwa tangu awali kufuatia uhusiano wa karibu na mastaa hao mtangazaji huyo, ambaye mshenga wake alikuwa ni mtangazaji wa kituo cha runinga cha Star TV, Sauda Mwilima.
Hii ni ndoa ya pili kwa mtangazaji huyo ambapo awali alikuwa ameolewa na Mohaned Mchopanga'Mchopsi', ambaye alizaa naye motto mmoja wa kike, kabla ya kuachana.
0 comments:
Post a Comment