Pichani juu ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akikabidhi funguo za gari mpya aina Corolla kwa Yohana Athumani Ntile wa Igunga Tabora aliyeibuka mmoja wa washindi wa promosheni ya Jivunie iliyomalizika hivi karibuni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mmoja wa maofisa wa Kitengo cha Masoko cha Airtel, Alice Paulsen. Airtel kwa sasa inaendelea na promosheni yake kabambe ya Kwanjuka ambayo mteja hutuma neno kwanjuka kwenda namba 15656 ambapo mteja anaweza kushinda shs milioni moja kila siku, tano mwisho wa wiki na shs milioni 50 mwisho wa promosheni. Picha inayofuata ni Yohana Athumani Ntile akipunga mikono mara baada ya kukabidhiwa gari lake.
Wednesday, July 27, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment