Social Icons

Sunday, May 1, 2011

ABIRIA WA KWENDA MIKOANI WAKWAMA

Abiria na wadau wengine wakiwa wamekusanyika kituoni hapo kufuatia mgomo huo.
ABIRIA waliotaka kusafiri kuelekea mikoani leo asubuhi walikwama kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (Ubungo Bus Terminal), kutokana na mgomo wa madereva waliokuwa wakidai mambo mbalimbali ikiwemo usumbufu wa maaskari wa usalama barabarani wanaobambikia makosa kwa ajili ya kutaka kuomba rushwa.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akipandisha suruali yake isichafuke na matope wakati akiingia eneo la tukio.


Baadhi ya madereva wakizuia basi, baada ya dereva mwenzao kuwasaliti na kuanza safari kinguvu, hata hivyo dereva huyo alipigwa mawe na vioo vya basi lake kuvunjwa ingawa lilifanikiwa kuondoka.


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga, akiwa na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela (nyuma yake) wakati wakielekea kwenye kikao cha usuruhishi.


Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwapa amri ya kutawanyika watu waliokusanyika bila sababu kwenye eneo hilo.


Mmoja wa abiria akiwa ameshika tama kufutia kutojua suluhu ya safari yake.

Watu wakiwa wamekusanyika kusubiri hatma ya mgomo huo.

Abiria wakiingia kwenye mabasi tayari kwa kuanza safari baada ya suruhisho kupatikana.

0 comments: