Hiace lenye namba za usajili T 908 BCM linalofanya safari zake Mikese kuja mjini Morogoro likiwa limeharibiwa vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na roli aina ya Scania lenye namba za usajili T 251 BBG lililokuwa likivuta tela lenye namba za
usajili T 812 BBP katika jijiji cha Mkambarani nje kidogo ya mji wa
Morogoro leo alfajiri.
MZIMU wa ajali za barabarani umeendelea kuuandama Mkoa wa Morogoro ambapo nyingine mbaya imetokea leo alfajiri na kusababisha vifo vya watu sita hapo hapo.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari aina ya Hiace lenye namba za usajili T 908 BCM linalofanya safari zake Mikese kuja mjini Morogoro kugongana uso kwa uso na roli aina ya Scania lenye namba za usajili T 251 BBG lililokuwa likivuta tela lenye namba za usajili T 812 BBP katika jijiji cha Mkambarani nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Mtandao huu ulifika haraka eneo la tukio na kushuhudia baadhi ya maiti zikiwa ndani ya gari la polisi tayari kwa kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku kundi la watu waliokuwa na huzuni wakijazana katika eneo hilo la tukio ili kutambua waliofariki dunia.
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa roli aliyehama upande wake na kulifuata Hiace.
Mtandao huu ulimshuhudia Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro,lbrahim Mwamakula akihangaika kwenye tukio hilo la ajali na hasa ikizingatiwa kuwa zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika mkoa wake.
0 comments:
Post a Comment