Social Icons

Sunday, March 27, 2011

TUZO ZA MUSIC KILLI AWARDS 2011

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi akikabidhi tuzo ya heshima kwa Shirika la Utangazaji la Habari Tanzania (TBC) kwa Joe Lugalabamu.
Mwanamitindo Khadija Mwanamboka (kushoto) pamoja na Producer Pancho Latino (wa pili kulia) wakimkabidhi tuzo ya Msanii Mpya anaechipukia Linnah ambaye pia alijinyakulia tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike.
Wachezaji wa Soka nchini,Juma Kasseja (kushoto) na Shadrack Nsajigwa (kulia) wakimkabidhi tuzo tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab Mzee Yussuf.
Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabele akitoa shukrani kwa wapenzi wa Muziki wa dansi na waandaaji wa Tuzo hizo muda mfupi baada ya kukabidhiwa tuzo ya Heshima.
Mzee Small Ngamba na Bi. Chau wakikabidhi tuzo kwa Producer Man Water mwakilishi wa 20% ambaye alijinyakulia tuzo 5 (tano),katika mchakato huo.Msanii kutoka THT, Elius Barnaba (kulia), akikabidhiwa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba.Joe Makini akijinyakulia tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop.Cpwaa akitoa shukrani za dhati kwa mashabiki wake walio mpigia kura na kuweza kupata tuzo ya Video Bora ya Muziki.Mbungu wa Viti Maalum CCM, Mh. Vicky Kamata (kushoto), akimkabidhi tuzo ya Wimbo Bora wa R&B , Ben Poul.Msanii wa vichekesho toka kundi la Orijinal Komedi, ambaye pia ni Mwanamuziki akitoa shukrani zake kwa mashabiki wake mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Wimbo Bora wa Asili Tanzania.Lady Jay Dee akiwa ameshikilia tuzo mbili alizojishindia, za Wimbo Bora wa Afrika Mashariki na Msanii Bora wa Kike.Mkurugenzi Mkuu wa Prime Time, Juhayna Kussaga pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja wakimkabidhi tuzo ya Mtunzi Bora Man Water kwa niaba ya 20 %.
Tuzo ya Rapa Bora wa Bendi ilienda kwa Khalid Chokoraa kama anavyoonekana hapa akiwa na Josee Mara pamoja na Kalala Junior wanaounda kundi la Mapacha watatu ambapo Bendi yao pia ilichukua tuzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili.
Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae ilienda kwa Hardmad.
JCB alijinyakulia tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop.
Antonio Nugaz,Ruben Ndege pamoja na Dataz katika pozi.
Banana Zorro, Diamond na Ali Kiba wakitoa shoo ya pamoja.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,Dr. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa BASATA,Ghonche Matelego wakifatilia kwa makini shughuli ya utoaji Tuzo.
Wadau,toka kulia ni Bosco Majaliwa,Baraka Msilwa,Albert Makoye pamoja na Omary Baraka.
Rais wa RBP,Mama Rahma Al Kharous pia alikuwepo kushuhudia tuzo hizo.
Alice na shosti yake katika pozi.


0 comments: