Social Icons

Sunday, March 13, 2011

MUSTAFA HASSANALI AALIKWA KWENYE ONESHO LA MAVAZI LA `ARISE MAGAZINE FASHION WEEK` NIGERIA

Baada tu ya kuzindua kwa toleo la kiafrika ndani ya Movenpick jijini Dar es salaam, mbunifu wa kipekee wa kiafrika toka Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa kushiriki katika maonyesho ya mavazi yanayojulikana kama ‘Arise Magazine Fashion Week’ yanayotarajiwa kufanyika tarehe 10 hadi 13 Machi 2011 ndani ya jiji la Lagos Nigeria.

‘Arise Magazine Fashion Week iliyoandaliwa na Nigeria’s this Day, inanatarajiwa kukusanya wabunifu mahiri wa Afrika wa ndani na waishio nje ya mipaka ya Afrika watakaoonyesha ubunifu wao, huku wakisindikizwa na wasanii maarufu wa muziki kama vile Dbanj, Keri Hilson, and Estelle.
Akizungumzia akiwa ndani ya jiji la Lagos Nigeria, Mustafa Hassanali alinukuliwa akisema kuwa “nimefarijika na kufurahishwa sana kuwa mmoja wa washiriki wa onyesho hili la ‘Arise Magazine’. Kuwa kwangu wa kwanza kwa mara nyingine tena kualikwa katika onyesho hili la wana wa Afrika kunaonyesha kukubalika kwangu kama mbunifu katika jamii ya mitindo kimataifa” alisema Mustafa Hassanali.

Mustafa Hassanali ataonyesha mavazi yake ya kiafrika yaliozinduliwa Dar es salaam tarehe 4 March katika onyesho la Mamma MIA kwa msaada wa Utepe Mweupe, toleo ambalo lililosanifiwa na uzuri wa Bara la Afrika, mg’ao wa miale ya asubuhi ya jua na machweo yake, ukarimu na ucheshi wa watu wake.

“kama hujapendeza, gauni lako halijameremeta, na halina mkia, hilo si gauni la Mustafa Hassanali, kama toleo langu hili nimetumia uhalisia wa kitanzania, khanga na kupambwa kwa thamani na hariri za hadhi.” alijigamba Mustafa Hassanali.

Arise Magazine Fashion Week’ itafanyika katika hoteli ya Federal Palace Ijumaa ya tarehe 11 Machi saa 9 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mustafa Hassanali, mbunifu na mjasiriamali anaeamini katika “never say die” anatumia kipaji na ubunifu wake katika kuijenga leo na kesho katika ubunifu.

Kazi za Mustafa Hassanali zimethaminika kimataifa, ameweza kufanikiwa kuonyersha kazi zake zimeonekana katika majukwaa tofauti ya mitindo kama vile, Fashion Business Angola, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Africa Collection in Douala, Cameroon, India International Fashion Week 2009, Naomi Campbell’s Fashion for Relief 2009, Arise African Fashion Week2009, Durban & Cape Town Fashion Weeks, Vukani Fashion Awards in Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashin Festival in Sicily, Italy, M’Net Face of Africa, Mozambique, Uganda na Kenya Fashion Weeks ambapo kwa pamoja yamemjengea kuheshimika sana.

0 comments: