Msanii huyo aliyeonekana kama shoga akinadi CD zake kwa wateja.
KIJANA mmoja msanii wa komedi toka jijini Dar es Salaam ambaye alifika mkoani hapa kwa lengo la kuuza CD zake, jana alisongwa na watu wakimhusisha na ushoga kufuatia mavazi ya kike aliyovaa na kutembea nayo katika mitaa ya mji wa Morogoro bila soni yoyote.
Baadhi ya wananchi waliamua kusitisha safari zao na kumzunguka kijana huyo ambaye aligoma kuhojiwa na mtandao huu kwa maelezo kwamba yuko bize na kazi yake hiyo ya kuuza CD.
Kijana huyo ambaye kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kufikiri ni mwanamke kwa alivyojipodoa na kuvalia nguo za kike pamoja na kuweka matiti na makalio ya bandia, alivuta umati wa watu kwa staili yake hiyo ya kujipodoa na kurembua macho na midomo kana kwamba anashiriki mashindano ya urembo.
Hata hivyo, uchunguzi wa mtandao huu ulibaini kuwa watu wengi waliomzunguka msanii huyo hawakuwa wanunuzi wa CD hizo bali walifika eneo hilo kwa lengo la kumshangaa msanii huyo kwa jinsi alivyojigeuza kuwa kama mwanamke.
Mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya watu wakimzomea 'live' huku wakimtolea maneno ya kejeli.
"Binafsi sina shida ya kununua CD zako kwa jinsi ulivyonichefua kwa kujipodoa. Tunawaona hata kina Joti wanajigeuza wanawake wanapokuwa kazini, wewe iweje utembee mitaani na mavazi hayo ya kike huku ukirembua macho kwani ungeuza CD zako bila kujirembuasigeuza?" alisikika mwananchi mmoja mwenye itikadi ya madhehebu ya dini ya Answari Suni akimshambulia kwa maneno hayo msanii huyo.
Hata hivyo, msanii huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, hakuonekana kujali maneno hayo na badala yake aliendelea kuzinadi CD zake hizo.
Hadi mtandao huu unaondoka eneo hilo la mtaa wa Makongoro, ulishuhudia watu wakizidi kujazana kumtazama kijana huyo ambaye alikuwa kioja.
....akiwa amezungukwa na umati wa watu.
.....akiwa ndani ya duka la vipodozi.
...akiuza CD zake kwa wateja waliofika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment