Na Wilbert Molandi
WAKATI Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikielekea ukingoni, wachezaji wa Yanga wamekata tamaa ya kuongeza mikataba mipya ya kuitumikia timu hiyo baada ya Mjumbe wa Bodi ya Udhamini, Yusuf Manji (pichani) kuachia ngazi.
Manji ambaye pia alikuwa mdhamini asiye rasmi aliyekuwa akiwalipa wachezaji wa Yanga mishahara na fedha za usajili, hivi karibuni aliachia ngazi kwenye klabu hiyo baada ya kutokuwapo maelewano mazuri kati yake baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga, morali ya wachezaji imepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia Manji kujiondoa madarakani katika muda huu kuelekea kipindi cha usajili.
Chanzo hicho kiliendelea kusema, wachezaji hao wamekuwa wakiishi kwa mazoea ya kusainishwa mikataba kwa makubaliano kati yao na mdhamini huyo.
“Wachache wanaojua ukweli wa wachezaji hao, baadhi yao kila msimu au wapya walisajili kwenye ofisi za Manji kwa makubaliano maalum kulingana na mikataba yao.
“Usajili huo alioufanya ametumia fedha nyingi kusajili wachezaji kama Ambani (Boniface), Chuji (Athumani Idd) na Shamte (Ally). Hao ni baadhi ambao walisajiliwa na yeye, hivyo lazima watachanganyikiwa kisaikolojia,” chanzo hicho kilisema na kuongeza:
“Hivyo kuondoka kwa Manji kunaweza kuifanya Yanga kushindwa kuwabakiza wachezaji ambao mikataba yao inaisha kwenye msimu huu, kama vile Chuji na wengine.”
Licha ya Manji kuwalipa mishahara na fedha za usajili, pia alikuwa akigharamia kambi ya timu hiyo. Kampuni ya TBL nayo inalipa kiasi fulani cha mishahara kwa wachezaji wa timu hiyo

0 comments:
Post a Comment