Hirizi, bastola, vito vya dhahabu na pochi alivyokutwa navyo jambazi huyo vikiwa mezani.
NA DUNSTAN SHEKIDELE,GPL MOROGORO
KATIKA hali isiyo ya kawaida kijana anayefahamika kwa jina la 'Juma Nature' mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam aliyeuawa na polisi mkoani hapa juzi Jumatatu kwa kudaiwa kuwa ni jambazi, amekutwa na hirizi kubwa ndani ya pochi yake.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Bi. Adolphina Chialo, aliuonyesha mtandao huu hirizi hiyo yenye rangi nyeupe iliyozungushiwa uzi mweusi juu.
"Baada ya kupekuwa mwili wa jambazi hilo tulikuta hirizi kubwa ndani ya pochi yake pamoja na bastola na baadhi ya dhahabu walizokuwa wamepora katika duka la sonara," alisema kamanda huyo.
Wachunguzi wa mambo walidai kuwa hivi karibuni majambazi wengi wamekuwa wakidaiwa kuwatumia waganga wa kienyeji katika kazi yao hiyo ya ujambazi.
"Unajua majambazi haya hudanganywa na waganga wa kienyeji kwamba wakipewa hirizi hizo hawawezi kukamatwa wakiwa katika kazi yao ya ujambazi," walisikika wakisema baadhi ya watu waliokuwepo katika tukio hilo.
Wednesday, March 2, 2011
JAMBAZI, MOROGORO, AUWAWA AKUTWA NA HIRIZI
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment