Wafanyabiashara wakiondoa masalia ya mabanda yao.
WAFANYABIASHARA wa soko la mitumba la Urafiki jijini Dar es Salaam, maarufu kama 'Big Brother' wameelezea kilio chao baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuwavunjia mabanda yao ya biashara usiku wa kuamkia leo. Wafanyabishara hao wamesema uvunjaji huo umewasababishia hasara kubwa ikiwemo kupoteza mali zao walizolaza sokoni hapo.
Mfanyabishara huyu akisalimisha furushi lake la mitumba alilolikuta.
Mama Lishe na mwanae nao wakisalimisha vitu vyao.
Maaskari waliokuwa wakilinda usalama wakisukuma gogo lililoingia barabarani kimakosa wakati wa uvunjaji.
0 comments:
Post a Comment