Social Icons

Wednesday, March 30, 2011

BENDI YA MASHUJAA KUTAMBULISHA WAPYA

BENDI ya Mashujaa Musica Aprili 1 mwaka huu inatarajia kufanya onyesho la utambulisho wa wanamuziki wake wapya waliojiunga na bendi hiyo wakitokea bendi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Mgahawa wa Hadees, Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis, alisema kuwa maandalizi ya onyesho la utambulisho wa wanamuziki limekamilika kwa asilimia 99 na aslimia moja ikibaki kuwa ni onyesho lenyewe litakalofanyika katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho.
Aidha alisema kuwa onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya, lakini pia ni maalum kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wa bendi hiyo na kuonyesha kile kilichowafanya kukaa kimya kwa kipindi wakijipanga zaidi.

“Tumejiandaa vilivyo kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa dansi ujio mpya wa bendi yetu iliyokuwa kimya kwa ajili ya kujipanga ili kuweza kwenda na wakati katika jukwaa la ushindani la Muziki wa dansi, na pia tumejitahidi kuongeza wanamuziki katika kila idara kuanzia waimbaji hadi wanenguaji ili kuweza kutoa burudani iliyokamilika kwa mashabiki wetu” alisema Mujibu.

Aliwataja wanamuziki hao wapya wanajiunga na bendi hiyo kuwani pamoja na, Kajo anayetoka katika Kundi la Boziboziana, Jimmy Adol kutoka kwa Koffee Olomide, Profa Kariakoo kutoka Kinshasa, Kama Simba Komilion, kutoka kwa Felix Wazekwa.Wengine ni Rapa mahiri Sauti ya Radi, Kelvin, Salma Shaban ‘Teketeke’ Mariam Lelapel na Corando wote kutoka bendi ya Diamondi Musica.

Katika onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi inayoongozwa na vijana watatu ‘Mapacha 3’, bendi yenye umri wa mwaka mmoja tangu ilipoanzishwa na kuweza kujizolea sifa kem kem baada ya kutwaa Tuzo mbili katika Kili Music Awards 2010, ambazo ni Tuzo ya Wimbo Bora wa bendi wa 2010 pamojana Tuzo ya Rapa bora wa bendi wa mwaka 2010.















0 comments: