KATIKA kuonyesha kwamba hana ubaguzi wa aina yoyote katika jamii, Mbunge wa jimbo la Mvomero Mkoani Morogoro, Amos Makalla, ameamua kumuajiri kijana mmoja mfupi ‘Emoro’ anayekwenda kwa jina la Michael Nchimbi, kuwa mlinzi wa nyumba yake iliyopo maeneo ya Kihonda Mkoani hapa.
Juzi mtandao huu ulitembelea nyumbani kwa mheshimiwa huyo na kukuta baadhi ya watu wakimshangaa mlinzi huyo aliyekuwa na silaha ya kirungu.
Akizungumza na Mwandishi wetu emoro huyo, Nchimbi (43) alidai kwamba anamshukuru Makalla kwa kumpa ajira hiyo.
“Kwa kilema hiki ni vigumu kwa watu wengine kuniamini na kunipa jukumu la ulinzi, kipekee namshukuru mheshimiwa Makalla kwa kunipa ajira hii, pia na toa wito wa watu wengine kuiga mfano huu kwa mbunge wa Mvomero,” alisema Nchimbi.
Hapa akimpigia saluti ikiwa ni ishara ya salamu ya heshima kwa bosi wake.
Hapa ni baadhi ya majirani na Makalla wakiomba kupiga picha na Nchimbi.
0 comments:
Post a Comment