Social Icons

Monday, October 25, 2010

KAHAKIKI MAPEMA JINA LAKO KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA

Hiki ni kisehemu cha karatasi chenye orodha ya majina (hayaonekani) ambao wanadaiwa hawakutimiza masharti ya kupiga kura,hata sijui itakuwaje kwa watu wa namna hii.

Baadhi ya wakazi wa Kawe kituo cha Tanganyika Packers wakihakiki majina yao kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume ya uchaguzi hivi karibuni,Baadhi ya wakazi wa Kawe waliojiandikisha kwenye kituo hicho wamelalamika kwa kutokuyaona majina yao kwenye orodha hiyo na kwamba hawajui la kufanya na kwanini tatizo hilo limetokea dakika za mwisho,kwani siku za uchaguzi ndio zinaelekea ukingoni.

0 comments: