Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibroad Peter Slaa ametajwa ana nafasi ya kushinda lakini mpaka ahurumiwe na CUF.
Kwa mujibu wa wanchi waliotuma maoni yao ofisi kwetu baada ya tafiti mbalimbali kutolewa, Slaa anahitaji huruma ya CUF kwa sababu chama hicho kina mtaji mkubwa wa kisiasa Zanzibar hususan Pemba.Wananchi hao walisema kuwa CUF pia kina matarajio ya kuvuna kura nyingi Mikoa ya Kusini hasa Lindi na Mtwara, hivyo CHADEMA kinahitaji huruma siku ya uchaguzi.
Walisema, ili Slaa apambane vizuri na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ni vema apate kura nyingi kutoka CUF.
“Kama CUF wengi wakimpigia kura Slaa basi upinzani utakuwa mkubwa kati yake na Kikwete lakini wakimpigia mgombea wao ni mtihani,” alisema Juma Hamduni wa Temeke, Dar.
Katika hilo, baadhi ya wananchi walisema kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ni kiungo anayeweza kutoa alama ya ushindi kwa chama kipi.
“Tatizo hapa ni katiba lakini ukweli ni kwamba CUF na CHADEMA walipaswa kusimamisha mgombea mmoja, lakini kila chama kinaogopa kumezwa na kingine. Ipo wazi kuwa mwaka huu Slaa ana nguvu kubwa ila kushinda Urais ni ngumu,” alisema Lameck Benny wa Sinza.
Kwa jumla, gazeti hili lilizungumza na wananchi mbalimbali ambao asilimia 90 kati yao, walisema Slaa atabanwa kwa sababu ya CUF hasa Zanzibar na Mikoa ya Kusini.

0 comments:
Post a Comment