Social Icons

Tuesday, September 7, 2010

'SPIDER DAN': MPANDA MAGHOROFA KWA NJE AKAMATWA

Dan Goodwin (Spider Dan) akikwea jengo la Millennium Tower katika Mtaa wa Mission.
MTU mmoja aliyeweza kukwea kwa nje jengo lenye ghorofa 58 na hatimaye kuipeperusha bendera ya Marekani alipofika juu ya jengo hilo, alijikuta amekamatwa.

Dan Goodwin (54), aliyelikwea jengo la Millennium Tower la San Francisco, alikamatwa na polisi. Jengo jingine alilowahi kulipanda ni Sears Tower la Chicago.

Katika kupanda kwake, alitumia vikombe vya plastiki vyenye kutoa hewa nje na kunasa kwenye kuta za jengo hilo lenye urefu wa mita 197 kwenda juu. Goodwin hakutumia kamba yoyote.

Alipuuza amri ya kumtaka asikwee jengo hilo na hata zimamoto walishindwa kumkamata kwa ngazi zao kwani alikwenda haraka sana.

Ilimchukua masaa matatu kufika juu ya jengo hilo.


Watu wakimshangilia Dan Goodwin wakati akielekea juu.

0 comments: