Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kulia), akiwaongoza wakuu wa vyombo vya habari kutembelea kiwanda cha sukari cha Kagera mwishoni mwa wiki iliyopita. Ziara hiyo ilifadhiliwa na NSSF ili kuona miradi mikubwa ya kiuchumi inayokopeshwa na mfuko huo wa jamii.
Meneja wa kiwanda cha sukari cha Kagera, mhandisi Nestory Rwechungura akiwaeleza wakuu wa vyombo vya habari jinsi kiwanda chake kinavyofanya kazi.
Wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakipata maelezo ya kitaalamu juu ya mafanikio makubwa ya kiwanda cha sukari cha Kagera katika umwagiliaji toka kwa meneja umwagiliaji wa kampuni hiyo, Laizer Morumo wakati wa ziara yao kiwandani hapo.
Wednesday, October 26, 2011
ILIKUWA HIVI ZIARA YA WAKUU WA VYOMBO VYA HABARI KAGERA
CHEKI MATUKIO YA AJALI KATIKA BASI LA DELUX KIBAHA
PICHA: FK BLOG
Tuesday, October 25, 2011
DK. KIKWETE AWASILI NCHINI AUSTRALIA
Rais Kikwete akiongozana na Mama Salma Kikwete amewasili mjini Perth tayari kujiunga na viongozi wenzake wa nchi za Jumuia ya Madola kwa ajili ya mkutano uliopangwa kuanza Ijumaa, Oktoba 28, 2011, katika ukumbi wa Riverside Theatre.
Kama ilivyo kawaida, Mkutano huo wa CHOGM ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, umetanguliwa na Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Nje za Jumuia ya Madola na wakati CHOGM inaendelea itakuwepo mikutano mingine ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Jumuia ya Madola wa Vijana, Mkutano wa Jumuia ya Madola wa Biashara na Mkutano wa Jumuia ya Madola wa Wananchi .
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano wa CHOGM tokea ashike madaraka ya kuongozwa Tanzania miaka sita iliyopita. Alishiriki mikutano ya CHOGM iliyofanyika mjini Kampala, Uganda, mwaka 2007, na mjini Port of Spain, Trinidad na Tobago, mwaka 2009.
Mbali na kuhudhuria Mkutano wa CHOGM, Rais Kikwete atatumia nafasi ya Mkutano huo kukutana na viongozi mbali mbali wa nchi na mashirika ya kimataifa ya sekta za umma na sekta binafsi.
Miongoni mwa shughuli zake za kwanza kesho, Rais Kikwete anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Jumuia ya Watanzania wanaoishi katika eneo la Australia Magharibi.
Keshokutwa, Rais Kikwete atakuwa mzungumzaji katika mdahalo kuhusu jinsi ya kuwawezesha akinamama ili waweze kuongoza – Empowering Women to Lead- ulioandaliwa na Mheshimiwa Julia Gillard, Waziri Mkuu wa Australia na mwenyeji wa CHOGM mwaka huu baada ya ameshikiri katika halfa kuhusu suala hilo hilo itakayoandaliwa na Mheshimiwa Quetin Bryce AC, Ganava Mkuu wa Australia (The Commonwealth of Australia).
Keshokutwa hiyo hiyo, Rais Kikwete pia atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa Jumuia ya Madola wa Biashara ambako atatoa hotuba maalum yenye mada: “Africa: Creating a New Economic Power for the 21st Century”. Siku hiyo hiyo, Rais Kikwete atakuwa mwenyekiti wa mkutano kuhusu suala la madini kati ya Tanzania na Australia wa “Tanzania-Australia Mining Roundtable” ambao utahudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara.
Miongoni mwa mambo makubwa yatayojadiliwa kwenye Mkutano wa CHOGM mwaka huu ni pamoja na viongozi wa nchi wanachama wa Jumuia kuangalia jinsi ya kuimarisha uwezo wa Jumuia katika kuunga mkono demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora miongoni mwa nchi wanachama waa Jumuia hiyo.
Mkutano huo pia utajadili jinsi ya nchi wanachama wanavyoweza kukabiliana na changamoto za sasa za kimataifa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uchumi endelevu, jinsi ya kuondokana na matatizo za sasa ya kiuchumi duniani na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Picha: Kwa Hisani ya Fullshangwe Blog
SALHA ESRAEL AANZA KUWATIA PRESHA MISS WORLD 2011
Miss Tanzania 2011, Salha Israel (mwenye nguo za njano), akifanya mazoezi ya viungo na baadhi ya washiriki wenzake waliofika kambini hapo tayari kwa Shindano la Urembo la Dunia litakalofanyika hivi karibuni jijini London Uingereza.
Saturday, October 22, 2011
Je, wadau wa MATEJA20 mnaizungumziaje tabia ya hawa mastaa kupima ngoma mara kwa mara hasa Sintah ambaye anarekodi ya kupima zaidi ya mara sita sasa tangu mwaka huu ulipoingia?
SWAHILI FASHION WEEK IN ANGOLA ON 15/10/2011
Designer Gabriel Mollel from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011
Designer Manju Msita from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011
Mustafa Hassanali from Tanzania during the Fashion Bussiness in Angola on 15th-oct-2011


















