Social Icons

Wednesday, September 28, 2011

AIRTEL TANZANIA NA ENGEN PETROLEUM ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI
Kamishna Mohamed Mpinga akionesha stika hizo za aina tatu kwaajili ya magari, pikipiki na bajaji ambazo mwaka huu zinaalama maalum ambazo haziwezi kugushiwa na mtu yoyote.

(kulia), ni Kamishna Mohamed Mpinga akionesha stika hizo tatu kwaajili ya magari, pikipiki na bajaji.Mkuu waMawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano akijaribu kuonyega uhalisia wa stika hizo.
Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kulia), akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo na Mjumbe wa baraza la Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo, akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Mkuu waMawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na Mjumbe wa baraza la Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu.
Baadhi ya wanahabari na wadau waliofika kwenye makabidhiano hayo wakifuatilia zoezi hilo kwa makini.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ya ENGEN kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.
Leo tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Bukoba. ENGEN Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya ENGEN kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa. Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 2,200 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .
Matokeo ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha jitihada hizi”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.

Note:

Umuhimu wa usalama barabarani hauwezwi kupuuzwa, kila siku tunashuhudia ajali nyingi zikisababisha kupoteza maisha, wa Tanzania wengi, uharibifu wa mali nyingi zenye thamani ya mamilioni. Zaidi ya mguso wa kibinadamu utokanao na ajali za barabarani lakini pia maafa na majeraraha yatokanayo na ajali za barabarani zinaleta athari za kijamii na kiuchumi. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu 2,850 wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani. Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kwamba watu 3,582 walipoteza maisha huku majeruhi wakiwa zaidi ya 20,000 wakati watembea kwa miguu na wapanda baiskeli wakiwa hatarini zaidi.

Mwaka 2010 katika jumla ya ajali 22,750 gharama au hasara iliyotokana na ajali za barabarani zinakadiriwa kufika bil 363. Hii ni athari kubwa kiuchumi.

Tuesday, September 27, 2011

HARUSI YA NARGIS MOHAMED FULL SHANGWE!!!Nargis Mohamed Jiwa (kushoto), akilishana keki kwa staili ya siku hizi na mume wake mpendwa Idd Issa Suleiman Romore, katika Ukumbi wa Stallion Kawe Over kado jijini Dar es Salaam.
Keki ilichukua nafasi namna hii kwa wapendanao hawa.
Hapa Nargis na mumewe wakinyweshana 'Shampeni' mara baada ya kufunguliwa na kuombwa kufanya hiyo ikiwa kama ishara ya ufunguzi wa vinywaji ukumbini hapo.
Nargis na mmewe wakiteta jambo na mmoja wa wanakamati wa sherehe hiyo.
... akimsaidia 'kusevu' chakula mumewe.
Mama mzazi wa Bibi harusi Mrs Batuli Wogole, akichukua matunda tayari kwa msosi wa usiku huo.
Msanii wa Filamu Bongo Sintah (kulia), akiwa kwenye pozi na maharusi hao, anaemfuatia ni Mboni Masimba na rafiki yao wa kwanza kushoto.
Mmoja wa watoto waliokuwa wakimwaga maua katika sherehe hiyo akiwa katika pozi na mama yake muda wa msosi.
Sintah, akijiandalia mazingira ya kuweka sawa tumbo lake.
Mambo ya msosi yalikuwa hivi mahari hapo.
Waarikwa wakijinafasi kwa raha zao.
... full maraha usiku huo!!
Mambo kama haya... ilikuwa kawaida kutokana na raha zilizokuwepo ukumbini hapo.
Unaona mtu kati... na kibao cha Katumba!!!
Raha ya harusi kujimwaya mwaya Bhanaaa...!
Nargis ... hakutaka kuboa sherehe yake bhana .... kwahiyo hakuwa nyuma kuzungusha nyonga yake mahari hapo.
Mambo ya Cheers...
Bi harusi akicheza miondoko ya 'kwaito' na waarikwa.
Maharusi wakiwa katika pozi na watoto waliokuwa wakimwaga maua.
Wakati maharusi hao wakiingia ukumbini.
Sintah, Mboni na rafiki yao katika pozi.
Sintah, akiwa katika pozi na Jacqueline Patrick.
Sintah alijiachia namna hii kabla ya kuzama ukumbini hapo.
Salma Msangi (wa pili kulia), akitoka kupakuwa msosi.
Jack nae hakuwa nyuma kujiandalia msosi mahari hapo.
Waarikwa wakigonga msosi
Watu walipozi kwa utulivu kama inavyoonekana.
Mambo ya msosi

SHEREHE ya ndoa ya kihistoria ya Miss Tanzania namba tatu 2003/04, Nargis Mohamed Jiwa aliyofunga na mfanyakazi wa benki moja maarufu jijini Dar es Salaam, Idd Issa Suleiman Romore, imevunja rekodi kufuatia mambo makubwa yalijitokeza katika shughuli hiyo.

Sherehe hiyo iliyoshuhudiwa na MATEJA20, hatua kwa hatua ilichukua nafasi mwishoni mwa wiki iliyopita Septemba 24, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa The Stallion uliopo Kawe, Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na waalikwa wa kada mbalimbali ndani na nje ya Bongo.

Kabla ya maharusi hao kutimba eneo hilo, wageni waalikwa walishuhudiwa wakiingia na magari ya kifahari ambapo kwa uchunguzi makini hakukuwa na mkweche hata mmoja wala teksi huku kila mtu akiwa amependeza ajabu.

Nargis ambaye pia ni staa wa muvi za Kibongo alizama ukumbini hapo akifuatana na mumewe Idd saa 2:45 usiku ambapo kiota hicho cha burudani kililipuka kwa shangwe na vigelegele kutoka kwa waalikwa na mashostito wake.

Baada ya mapokezi hayo, Nargis aliyekuwa akimeremeta kama nyota aliongozana na mumewe hadi meza kuu na ndipo ratiba ya shughuli hiyo ikaanza kufuatwa rasmi.

Shughuli hiyo ilianza kwa wanandoa hao wapya kufungua ‘shampeni’ kisha wakakata keki na kutumia muda wa kulishana keki kufanya utambulisho wa wageni wa pande zote mbili huku vinywaji vya bei mbaya vikiendelea.

Kabla ya kujisogeza kwenye meza ya maakuli, wanandoa hao waliburudisha kwa muziki kidogo kisha wakarejea meza kuu kuendelea na ratiba ya shughuli hiyo.

Baada ya utambulisho na muziki kidogo, muda wa msosi uliwadia ambapo wanandoa waliwaongoza waalikwa hadi meza ya chakula.

Watu waligonga maakuli ya maana yaliyosheheshwa na nyama za kumwaga za kupikwa, kuaangwa na kuchoma.

Muda mwingi Nargis aliyeuza nyago kwenye Filamu ya Yellow Banana alionekana kuchangamka kupita maelezo na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuonekana ‘beneti’ na mumewe huyo.

Mastaa wa Kibongo waliohudhuria waliongeza utamu kwa namna walivyopendeza na kuifanya sherehe hiyo kuonekana ya kifahari.

Baadhi ya mastaa hao ni pamoja na muigizaji Christina Manongi ‘Sintah’ modo Jacqueline Patrick, watangazaji Salima Msangi, Sakina Lyoka na Miss Mbeya wa miaka ya nyuma, Mboni Masimba.

Baada ya zawadi na shughuli zote huku maharusi wakizunguka kila meza kuwapa waalikwa mkono wa heri, walifungua muziki wa kufa mtu na kuserebuka muziki wa maadhi ya Kwaito.





TWANGA PEPETA, BI KIDUDE WAPAGAWISHA TAMASHA LA SANAA BAGAMOYOWanamuziki wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta' wakiwajibika stejini hapo jana kwenye Tamasha la miaka 30 ya Sanaa na Utamaduni lililofunguliwa katika Ukumbi wa Sanaa Bagamoyo Pwani.
Mkongwe wa muziki wa Mwambao nchini Bi Kidude, akitumbuiza kwenye tamasha hilo usiku wa kuamkia leo.
Wanenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwajibika jukwaani hapo.
Kikundi cha Muziki wa Mwambao kilichokuwa kikitumbuiza na Bi Kidude.
Mrembo akipiga kinanda katika tamasha hilo.
Bi Kidude (kulia), akiokota fedha alizotunzwa na mashabiki wake wakati akiimba.
Wananamuziki hao wakiwajibika jukwaani.

Mmoja wa wanamuziki hao akiwajibika.

Bi Kidude (kushoto), akisalimiana na kiongozi wa wanamuziki wa Twanga Pepeta Luiza Mbutu (kulia), katika ni mmoja wa wanenguaji hao akifuatilia maongezi hayo.
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta Mwijuma Mumini (kushoto), akisalimiana na Bi Kidude.
Kiongozi wa wanenguaji wa kike wa Twanga Pepeta Lilian Internet, akijitetea baada ya kubanwa mkono na Bi Kidude, baada ya kukawia kumsalimia.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakiwa katika pozi.
Maria Soloma (kulia), akibadilishana mawazo na Sabrina Mathew kwenye chumba cha mapumziko.
Mpiga Drums wa Bendi hiyo Yahya Omar, akiwa katika moja ya jukum lake.
Mpiga gitaa la Bass wa bendi hiyo Kado, akijaribu kumchezea lafu mke wa mkuu wa wanenguaji wa bendi hiyo Super K.
Super K (kushoto), akimkoromea kiaina Kado baada ya kumkuta akichezea mali yake.
Muimbaji wa Twanga Pepeta Dogo Rama akiwajibika.

BENDI ya African Stars International ‘Twanga Pepeta, na Mkongwe wa muziki wa Mwambao Bi Kidude, usiku wa kuamkia leo walifanya makamuzi ya kufa mtu katika Tamasha la Miaka 30 ya Sanaa na Utamaduni lililoanza tangu Septemba 26 mwaka huu na linatarajiwa kuisha Oktoba mosi mwaka huu katika Ukumbi wa Sanaa Bagamoyo.