Social Icons

Wednesday, January 26, 2011

VODA YAZINDUA BIDHAA YA WAREMAVU WA MASIKIO NA MACHO

Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionyesha simu maalum kwa waandishi wa habari ambayo kampuni hiyo imeizindua leo kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia Kushoto ni Meneja mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya na kulia ni Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Mgope Kiwanga.
Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa Vodacom Tanzania Mgope Kiwanga(kulia) akimkabidhi simu mwandishi wa habari wa gazeti la The African Sylvester Joseph aliyejishindia Bahati nasibu mara baada ya kampuni hiyo kuzindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Said Mtulya akionesha simu yake aliyojishindia katika bahati nasibu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kuzindua simu hizo maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia,anayeangalia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard.

Na Mwandishi Wetu
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na wenye matatizo ya kusikia.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya, alisema Jijini Dar es Salaam, simu hizo ni tofauti na nyingine kwa kuwa zitawawezesha wateja wao wenye matatizo ya kuona na kusikia kupata huduma ambazo hazipo katika simu za kawaida.

Alizitaja baadhi ya huduma hizo maalum zilizopo katika simu hiyo ni pamoja na maandishi makubwa katika Keypad zake, sauti kubwa katika spika zake na king'ora maalum nyuma ya simu kitakachowawezesha wateja wao kukibonyeza wakati wa dharura.

"Simu hizi za aina yake zitawawezesha wateja wetu wenye matatizo kama hayo kupata huduma ambazo hazipatikani katika simu nyingine za kawaida, natoa wito kwa watanzania wenye matatizo kama hayo kuzichangamkia simu hizi" Alisema.

Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni S306 ZTE ambazo zitapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama Vodashop au kwa mawakala wa Vodacom waliopo nchi nzima.

"Tumeamua kuja na simu hizi baada ya kugundua kuwa kuna watanzania wengi wanapata matatizo na simu nyingi kutokana na maandishi madogo, sauti ndogo, na kadhalika. Lengo ni kuwasaidia na kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kupata huduma za msingi kwa kutumia simu zao za mkononi bila vikwazo vyovyote vidogovidogo," Alisema.

Alisema kwamba simu hizo zinaweza kutumiwa hata na wasioona kwani ikibonyezwa herufi hutoa sauti inayo kujulisha umebonyeza herufi gani. Hivyo basi ni simu maalum kwa watu maalum katika jamii yetu.

Vodacom Tanzania imekuwa ya kwanza hapa nchini kubuni huduma mbalimbali kwani mbali na simu hiyo,Vodacom mapema mwaka jana ilizindua simu inayotumia mionzi ya jua ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi mbalimbali ambao wanapata matatizo ya miundo mbinu ya umeme.

Vodacom pia imewarahisishia mamillioni ya watanzania kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa, huduma inayowawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi.

Mbali na kutuma pesa kwa ndugu na marafiki wanao tumia mtandano wa Vodacom. Wateja wana watumia jamaa walio katika mitandao mingine hapa nchini.

Alimalizia kwa kusema, leo tuna furaha kuwawezesha wateja wetu kuchati bure kwenye mitandao ya Face Book, the grid na Vodamail. Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha huduma zetu mara kwa mara kwa ajili ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.

Euroleague Basketball live on SuperSport on DStv

After four months of gruelling regular season action, the 2010/11 Euroleague Basketball season has entered its second stage, the top 16. SuperSport, the World of Champions, will broadcast live matches across the African continent every Thursday night for the remainder of the season.

With games one of the top 16 just about complete, the league is taking on the all too familiar pattern of the top teams setting the pace in their respective groups.

Real Madrid, Panathinaikos, Fenerbahce Ulker and Regal FC Barcelona top the four groups and are expected to do so right into the third stage of the season, the quarterfinal round.

Starting on Thursday, SuperSport will broadcast live Fenerbahce Ulker Istanbul’s visit to Spain to take on Power Electronics Valencia in a group H encounter. Both teams are yet to taste Euroleague glory - Fenerbahce’s best placing was the quarterfinals, which surprised many, and Valencia’s entry into the top 16 is their best showing yet - will want to upset the applecart by surprising all and going all the way to winning the league.

The match is live on SuperSport 7A, 7N and Maximo2 at 10.40pm (EAT) with a repeat on SS 2A on Saturday at 6pm (EAT).

Sports across the world is not complete without African flair, and the Euroleague is no exception with Central Africa Republic’s Romain Sato, Nigeria’s Benjamin Eze and the Senegal duo of Boniface N'Dong and Pape Sow flying the African flag.

In February, Partizan Mt:S Belgrade, Montepaschi Siena, Union Olipija Ljubljana, Maccabi Electra Tel Aviv and Olympiacos Piraeus will headline SuperSport’s live broadcast of Europe’s premier basketball competition on Thursday nights.



WAZIRI AKERWA NA MADANGURO SHULENI



NAIBU waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi,Goodluck Ole Medeye amekerwa na wingi wa madanguro na vibanda vya kuonyesha picha za ngono vilivyoizunguka shule ya sekondari Enaboishu.

Ameuagiza uongozi wa kijiji , kuhakikisha kuwa ndani ya wiki moja wanaondoa madanguro,vijana wanaovuta madawa ya kulevya na vibanda vya kuonyesha picha za ngono,haraka iwezekanavyo kwani vibanda hivyo vinachangia wanafunzi wa shule hiyo kushindwa kuingia madarasani na kuishia kwenye vibanda hivyo .

Ole Medeye ambaye alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 12 ya kumaliza kidato cha 6 yaliyofanyika katika shule hiyo , mbali na agizo hilo alimtaka mkuu wa shule hiyo,Lession Ole Saking'oi kudhibiti nidhamu na kuhakikisha wanafunzi hao hawashiriki vitendo vichafu shuleni hapo.

Naibu waziri huyo alishtushwa na taarifa hiyo baada ya kuisikia katika risala iliyosomwa na wanafunzi wa shule hiyo , ikibainisha kwamba, vibanda hivyo vya ngono vimekuwa kero na vimechangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili kwa wanafunzi wa shule hiyo ,kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uzio unaozunguka eneo la shule.

Mmoja wa wanafunzi hao ambaye ni kiongozi wa wanafunzi hao ,Shangwe Alex alimwambia mgeni rasmi kuwa amelazimika yeye na wenzake kuushauri uongozi wa shule hiyo wakipendekeza, wanafunzi wa kike wabadili mavazi yao badala ya kuvaa sketi na shati pekee ,wawe wanavaa suruwali ndani ya sketi.

Alex alisema kuwa hali hiyo baada ya uongozi kutafakari na kukubali imesaidia kwa kiasi kikubwa kurudisha heshina na nidhamu kwa wanafunzi wa kike .

Awali wawanafunzi wa kike walikuwa wakivaa sketi fupi kupita kiasi na kuacha sehemu kubwa ya maungo yao wazi, kutokana na kujihusisha zaidi na kuangalia picha za utupu na kujikuta wakishawishika kufanya ngono na wanafunzi wenzao wa kiume na vijana wanaoishi jirani na eneo hilo na kusahau wajibu wao wa kusoma.

Aidha kwa upande wa mkuu wa shule hiyo,Mwalimu Saking'oi pamoja na kukiri kuwepo kwa vibanda hivyo vya ngono,ameahidi kushirikiana na uongozi wa eneo hilo kuhakikisha vinaondolewa haraka iwezekenavyo.

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 128 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika shule hiyo.

Monday, January 24, 2011

STEVE RnB ALBUM YAKE YADATISHA KITAA




MLALAMIKAJI KESI YA JERRY MURO AKIRI KUTOA RUSHWA


Michael Wage akiondoka mahakamani baada ya kukiri kutoa rushwa ya shilingi milioni 10.
Na Richard Bukos
ALIYEKUWA Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage, ambaye kwa sasa ni mlalamikaji na shahidi wa kwanza katika kesi ya kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili mtangazaji wa kituo cha luninga cha Taifa (TBC1), Jerry Muro, amekiri kutoa rushwa ya kiasi hicho cha pesa.

Wage alisema hayo baada ya kubanwa na wakili wa upande wa utetezi, Majura Magafu, aliyemtaka kuelezea lengo la kutoa shilingi milioni moja alizodai kuwapa Jerry Muro na wenzake.

Mlalamikaji huyo alisema aliwapa Jerry Muro na wenzake kiasi hicho fedha ili wasirushe hewani kwenye kipindi cha ‘Usiku wa Habari’ tuhuma za matumizi mabaya fedha kwenye Halmashauri ya Bagamoyo.

Magafu alimueleza Wage kuwa kitendo chake cha kueleza mahakamani kuwa alitoa rushwa ili tuhuma zake zisirushwe kwenye luninga kinathibitisha kuwa mlalamikaji huyo ana kesi ya kutoa rushwa, hivyo kosa hilo linaweza kumpeleka jela.

Kesi hiyo iliyounguruma leo inatarajiwa kuendelea tena mahakamani hapo kesho, Jumanne, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Mirumbe.



Jerry Muro, akiondoka mahakamani.


...Akibadilishana mawazo na wakili wake, Richard Rweyongeza (kushoto).

MATAYARISHO KILI MUSIC AWARDS YAIVA


George Kavishe akiongea jambo na waandishi wa habari.
MCHAKATO wa utoaji tuzo za wasanii nchini zinazojulikana kama ‘Kili Music Award’ ambao huendeshwa kila mwaka na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), leo umeendelea na maandalizi ya utoaji wa tuzo hizo.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam, Meneja wa TBL, George Kavishe, alisema mwaka huu kampuni hiyo itatumia wanamuziki wa ndani katika usiku wa utoaji wa tuzo hizo.

Kampuni hiyo itashirikiana na Basata ili uboresha zaidi burudani ya mwaka huu.




Mratibu wa tuzo wa Basata, Angela Luhala, akifafanua jinsi utaratibu wa utoaji tuzo utakavyokuwa.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

WASANII WAPEWA ELIMU YA SANAA,

Mgunga Mwa Mnyenyelwa (aliyesimama kushoto), akitoa ufafanuzi juu ya tamthiliya ya “Nguzo Mama” inayotarajiwa kuonyeshwa tarehe 28 na 29 Januari mwaka huu kwenye ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi.
WASANII mbalimbali wakiwemo wacheza filamu, wachoraji, wanamuziki na wachongaji vinyango na sanamu, leo wamepata elimu ya sanaa ya maonyesho na kuhamasishwa kupima afya zao na jinsi ya kuepuka kukumbwa na ugonjwa wa ukimwi.

Akizungumza katika hafla ya Jukwaa la Sanaa lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, Mgunga Mwa Mnyenyelwa, amewataka wasanii wote kuwa na dira katika kazi zao kabla ya kutoa kazi akawataka wafanye utafiti ili kujua kile wanachokifanya kama kitanufaisha taifa

Aidha aliendelea kusema kuwa kikundi hicho kina malengo ya kuwasaidia wasanii wa Bongo Fleva ili waweze kuimba nyimbo zao zikiwa na mguso wenye asili ya Kiafrika kwa lengo la kuzitofautisha na za nchi nyingine.

Naye, mshauri kutoka shirika la AMREF, Bahati Mwitula, aliwapa somo wasanii hao na kuwahamasisha kupima afya zao ambapo alisema kuwa shirika hilo limeamua kuwafuata watu pale walipo na siyo mpaka watu wawafuate wao.



Wasanii wakisikiliza kwa makini mafunzo.

Bahati Mwitula (aliyesimama) akijitambulisha kwa wasanii.

……Akifafanua jambo kuhusu ukimwi.