Social Icons

Saturday, December 3, 2011

FALLY IPUPA APAGAWISHA USIKU WA KIAFRIKA DAR !

Fally akinengua na mrembo jukwaani.
Fally Ipupa akiwajibika jukwaani hapo.
… akiserebuka na mrembo mwingine.
… akiserebuka na mrembo mwingine.
: Baadhi ya wanamuziki wa Fally Ipupa
: Msanii wa filamu Bongo, Steven Kanumba ‘akizama’ ukumbini hapo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Ali Kiba (kulia), akikamua katika shoo hiyo na Dully Sykes.


Mmoja wa wasanii waliotumbuiza ukumbini hapo akionyesha mazingaombwe, na hapa akiwa amemlaza hewani mwenzake aliemtia usingizi na kupaki akiwa ameegemea kichwa tu.
Msanii huyo akionyesha kumlaza mwenzake kwenye viti.
: … akiwa amemlaza katika ubao uliokuwa juu ya viti kabla ya kuvitoa.

Wasanii wa sarakasi wakionyesha uwezo wao.


Kuwa hivi yanahitajika mazoezi ya nguvu.


Fally Ipupa akimkokota mrembo kumuondoa stejini hapo.


Mboni Masimba (kushoto) na rafikiye wakipiga makofi.


Kanumba akiwa katika pozi na mrembo.



Baadhi ya mashabiki wakiofrika ukumbini hapo wakifuatilia shoo hiyo.

MSANII wa muziki wa Dansi kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Fally Ipupa, usiku wa kuamkia leo amepagawisha vilivyo katika Tamasha maalum la Usiku wa Kiafrika lililokuwa limeandaliwa na Club E ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, huku akisindikizwa na Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Bendi ya THT.

Tamasha hilo lilikuwa hususani kwa kuonyesha uafrika zaida ambapo baadhi ya vitu vilivyokuwa vikionyeshwa ukumbini hapo ni pamoja na mavazi ya kiasili ya mwafrika na michezo mbalimbali yenye tamaduni ya Kiafrika.



SIKU CHACHE BAADA YA KUACHIWA HURU JERRY MURO AKABIDHIWA TUZO YA MWANDISHI BORA


Baraza la Habari Tanzania (MCT), limekabidhi Tuzo kwa Mshindi wa Jumla wa Uandishi bora kwa mwaka 2009, aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro ikiwa ni baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake wawili.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Kajubi Mkajanga, alisema tuzo hiyo imeambatana na fedha taslimu shilingi milioni 6 na laki mbili na kuwa walishindwa kuitoa mwaka huo kutokana na Mshindi huyo kukabiliwa na kesi ya kuomba Rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wange.

Kwa upande wake Mshindi huyo Bwana Jerry Muro , ameishukuru MCT, na kuwataka waandishi wa habari kushirikiana na kutokata tamaa pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali katika majukumu yao.
Picha: Habari na Matukio Blog

Thursday, December 1, 2011

ZANZIBAR HEROERS YAAGA MASHINDANO YA TUSKER CHALLENGE CUP 2011
Mchezaji Amir Hamad wa Zanzibar Heroers akimtoka mchezaji wa timu ya Somalia Kassim Ali Mursal wakati timu hizo zilipopepetana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika michuano ya kombe la Tusker Challenge Cup 2011.
Mchezaji wa timu ya Somalia Abdi Azizi(kushoto), akichuana na mchezaji wa timu ya Zanzibar Heroers Juma Othman wakati wa mchezo huo.
Khalid Ali Maursal wa timu ya Somalia akiruka juu kuokoa mashabulizi kutoka kwa washabuliajiwa timu ya Zanzibar Heroers.
Amir Hamad wa Zanzibar Heroers (kulia), akichuana na Kassim Ali Mursal wa Somalia katika kuwania nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya Tusker Challenge Cup