Social Icons

Friday, June 3, 2011

NYERERE DAY IN KAMPALA UGANDA


By Paul Mallimbo, Kampala

PRESIDENT Yoweri Museveni, has said that the former Tanzanian President, the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, is the greatest black man who has ever lived.

The President was on 1st June paying his tribute to the late Tanzanian leader during a church ceremony held at Namugongo Basilica, the Uganda Martyrs’ Shrine near Kampala to mark the 5th Julius Kambarage Nyerere Day. The day is marked annually to pray for the repose of the soul of the late Mwalimu so that the church recognizes to be acknowledged a Servant of God towards the cause of his beautification. The 1st of June, acknowledged as the Namugongo Nyerere Day, lays emphasis on prayer in order to spread the cause of the beatification of Mwalimu to the whole world.

The day attracted believers from Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi and other countries as they also prepare for the annual Uganda Martyrs’ Day celebrations that take place on 3rd June.

President Museveni noted that the former Tanzanian leader practiced his Christian faith here on earth by taking care of the lives of people. He also said that Nyerere spearheaded the political and spiritual struggle as well as the promotion of education. He added that Nyerere was a pioneer in the struggle for economic emancipation of the African continent. Mr. Museveni, therefore, lauded him for establishing Dar - es - Salaam University and for launching free education in the United Republic of Tanzania. He expressed happiness to note that Africa is getting out of darkness through the promoting of education.

Regarding the Namugongo grounds, President Museveni said that it is an area of a spiritual struggle and reminded the congregation that the Christian religious believers were, at the time of the martyrdom of the Christian converts, in conflict with some of the bad practices of the traditional leaders in Buganda.

President Museveni pledged that “we shall continue coming to Namugongo to pray for the beautification and finally for Mwalimu’s canonization. If we continue knocking and asking, Rome will open for us.”

He was happy to see that the people of Tanzania have continued to come to pray for Mwalimu Nyerere’s beautification.

Bishop Emeritus, Rt. Rev. Edward Baharagate, who was the main celebrant said that Mwalimu Nyerere is a servant of God and that the church is in the process of beatifying him.

The Tanzanian Prime Minister, Mr. Mizengo Peter Pinda, in a speech read on his behalf by State Minister Ms. Mary Michael Nangu, saluted President Museveni for sparing time to attend the intersession prayer at Namugongo for Mwalimu Nyerere.

He commended Mr. Museveni and other Ugandans for recognizing the contribution of Mwalimu towards the welfare of mankind. He said Mwalimu’s case of beatification was beyond Tanzania.

Speaking on behalf of the Nyerere family, Mr. Charles Makongoro Nyerere thanked President Museveni and other Ugandan Christians for their hospitality during their numerous visits to Uganda.

Rev. Fr. Alfred Kwene, who represented Bishop Michael Msonganzila of Musoma Diocese, congratulated the people of Tanzania for producing a President who is blessed.

At the same occasion, the Mayor of Kira County, Mr. Mamerito Mugerwa said it is God who chooses leaders and He is the one who chose President Museveni. He prayed to God to give blessings to the late Mwalimu Nyerere.

Mary Nagu and Mama Maria Nyerere (L)
Uganda resident.


EXTRA BONGO USIKU DAR KUAMKIA LEO


Kiongozi Extra Bongo, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’, akiserebuka sambamba na mrembo mfupi aliyejulikana kwa jina la Kadisa Jacob.

Mnenguaji maarufu, Hassan Said ‘Super Nyamwela’, akiwaongoza mashabiki kucheza moja ya mitindo inayotumiwa na bendi hiyo.

Shabiki wa muziki akifanya vitu vyake.

MAHAKAMA YAAMURU MBOWE AKAMATWE

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imetoa amri ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe popote alipo na kufikishwa mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutotii amri ya kufika mahakamani hapo.

Mahakama hiyo pia imemtaka mdhamini wa Mbowe aliyetajwa kwa jina la Julius Isaya Magwe, kufika mahakamani hapo mara moja ili kuieleza mahakama hiyo sababu za kutotii amri ya mahakama pale anapohitajika.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Charles Magesa alisema jana kuwa kimsingi Mahakama inakubaliana na hoja ya wakili upande wa Serikali kuitaka mahakama kutoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe kwa sababu ya kutotii amri ya kufika mahakamani au kumtuma mdhamini wake.

Alisema sababu iliyotolewa mahakamani hapo kwamba mshtakiwa huyo ni mbunge na yupo kwenye vikao vya Kamati za Bunge haina uzito kwa kuwa hiyo ni moja ya shughuli zake kama ilivyo shughuli nyingine kwa watumishi wa serikali.

“Hivyo basi kama ni shughuli zake za kawaida, haimzuii kutii amri ya mahakama pale anapoitwa bila kujali anaitiwa nini,” alisema Magesa.

Hakimu Magesa alisema kuwa anachokumbuka ni kwamba Mahakama hiyo kweli ilipokewa maelezo ya kuwa washtakiwa hawatahudhuria mahakamani hapo Mei 27 mwaka huu kwa sababu ya kuwa katika vikao vya Kamati za Bunge na kuagiza waje wadhamini wao siku kesi inapotajwa. Ndiyo sababu Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini alimpeleka mdhamini wake mahakamani hapo.

Lakini, kabla ya kuhitimisha agizo hilo, hakimu huyo, awali alitoa amri ya kutaka kukamatwa kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philimon Ndesamburo, ambaye naye hakutii amri ya mahakama kwa kutofika Mei 27, 30 na 31 na hata jana.

Hata hivyo, baada ya kutoa amri ya kukamatwa kwa Ndesamburo ambaye naye ni mshtakiwa, ghafla alijitokeza mdhamini wake, Rubeni Ngowi na kuiambia mahakama hiyo kuwa alikuwapo Mei 30, ila hakuweza kusogea mbele kwa sababu ya woga wa mahakama na kwa kuwa hakuitwa.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Magesa alimhoji mdhamini huyo akitaka kujua alikuwa wapi Mei 27 mwaka huu kesi hiyo ilipotajwa. Ngowi alijitetea kuwa alikwenda jijini Dar es Salaam kwa familia yake ambayo ilikuwa ina matatizo, lakini Mei 30 alifika mahakamani hapo na kuomba kuondoa amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa wake.

“Basi kwa sababu nakumbuka ulikuwapo Mei 30 na nilikuona hapa mahakamani ukimnong’oneza wakili Kimomogoro, basi naondoa amri hii. Ila naomba utii amri ya mahakama pale mshtakiwa anapokosa uje kutoa sababu za kukosa kwake,” alisema Magesa.

Hakimu Magesa pia alitoa onyo kwa washtakiwa wengine wakiongozwa na Dk Willibrod Slaa wasiache kufika mahakamani, kila siku kesi yao inapotajwa na pale wanapokuwa na sababu ya kutofika, wahakikishe wadhamini wao wanakuwapo kutoa sababu za kukosekana kwao.

Akitoa uamuzi wa hatima ya dhamana za washtakiwa wa kesi inayowakabili viongozi wa Chadema, Godbless Lema, Joseph Selasini na wafuasi wao, Hakimu Mkazi Magesa, alisema Mahakama hiyo imeondoa hati ya kukamatwa kwa washtakiwa hao kama ilivyoamriwa awali na kutupilia mbali ombi la wakili wa serikali la kutaka wafutiwe dhamana.

Alisema kuwa kutokana na kupitia kwa makini maelezo ya utetezi wa pande zote mbili kwa Wakili wa Serikali, Edwin Kakolaki na wakili upande wa utetezi, Medhod Kimomogoro, Mahakama hiyo imeamua kuwapatia dhamana ya kudumu washtakiwa ambao ni Dk Slaa na wenzake, kwa kutii amri ya Mahakama.

“Mahakama hii imeamua kufuta amri ya dhamana ya muda na kuacha dhamana ya awali kwa sababu mara mahakama hii ilipotoa amri ya kuwakamata Mei 27 mwaka huu, washtakiwa hao walifika mahakamani hapa kujisalimisha wenyewe na wengine, akiwamo Mbunge Joseph Selasini, alituma mdhamini wake, hivyo nawaachia dhamana zao,” alisema Magesa.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Serikali, Januari 5 mwaka huu ambapo washtakiwa 19 walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka la kufanya kusanyiko pasipo na kibali na kutoa maneno ya uchochezi. Washtakiwa walikana makosa yao na kwa sasa wako nje kwa dhamana hadi Juni 24 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Kauli ya Mbowe
Akizungumza na Mwananchi jana jioni, Mbowe alisema anatarajia kutoa tamko kuhusu suala hilo leo saa tano asubuhi jijini Dar es Salaam, lakini alikataa kutaja ni wapi mkutano wake na waandishi wa habari utafanyika.

“Nitatoa tamko kesho, lakini nasikitishwa na tafsiri hii ya Mahakama kwamba mimi nimekaidi amri ya kufika katika vikao vya mahakama. Nasema hivyo kwa sababu mara ya mwisho tulipokuwa mahakamani, tulipewa ruhusa ya kuhudhuria vikao vya Kamati za Bunge,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Sasa sijui tafsiri yake ni nini, lakini niseme tu kwamba haya yote kuhusu sakata la Arusha na amri za polisi kuwakamata wabunge wa opposition (upinzani) nitalizungumza kesho (leo) kwa vyombo vya habari”.

Kwa mujibu wa Mbowe, waliomba ruhusa ili kuwawezesha kushiriki vikao vya Kamati za Bunge kutokana na umuhimu wa masuala ya bajeti kwa umma ambayo pia yanawagusa mahakimu na Idara ya Mahakama kwa jumla.

“…hebu kama mnakumbuka, katika Bunge lililopita tulijadili ule muswada wa sheria unaogusa idara ya mahakama sisi wabunge wa upinzani tulitumia nguvu kubwa kuwatetea mahakimu katika mambo mengi. Sasa katika suala hili la bajeti si vizuri tukikosekana kwenye vikao na ndiyo maana tuliomba ruhusa siku ile na tukaruhusiwa, ”alisema Mbowe.

CHANZO:MWANANCHI JUNI 03,2011

Thursday, June 2, 2011

BASI LA ABOOD LAJERUHI WATU 30

Dereva wa basi la Abood lililopata ajali.

Mmoja wa wauguzi wa wodi ya wagonjwa mahututi akimhudumia mmoja wa majeruhi Gosbert Kajalaba aliyevunjika miguu yote miwili na mkono.

Na Thompson Mpanji, Mbeya
WAKATI bado Watanzania wakiendelea na majonzi na kuomboleza vifo vya watu 16 waliofariki dunia katika ajali ya basi la abiria la kampuni ya Sumry iliyotokea wiki iliyopita maeneo ya Igawa, mpakani mwa Iringa na Mbeya, watu wengine 30 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la Abood lenye namba za usajili T 297 ATH lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya jana katika eneo la Mlima Nyoka, Itewe, katika barabara ya Mbeya-Iringa.

Akiongea na mtandao huu ofisini kwake mkuu wa kitengo cha upasuaji, Dkt. Chrispin Masandika kwa niaba ya mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya amesema majeruhi hao walipokelewa jana (Juni Mosi) majira ya usiku ambapo mgonjwa mmoja Gosbert Kajalaba (45), mkazi wa Dar es Salaam mtaalam wa masuala ya hoteli aliyekuwa akifika kutoa semina katika hoteli ya Rift Valley yupo mahututi baada ya kupata jeraha kichwani, kuvunjika miguu yote miwili na mkono wa kushoto.

Dkt. Masandika amesema baada ya kumfanyia upasuaji usiku anaendelea vizuri ambapo dereva wa gari hilo George David (45), mkazi wa Dar es Salaam amelazwa katika wodi namba moja akiendelea na matibabu huku majeruhi wengine wanane wakiwa wamelazwa na kuendelea na matibabu na wengine 20 kuruhusiwa kurudi majumbani baada ya kupata matibabu.

Mmoja wa majeruhi aliyelazwa katika wodi namba moja aliyejitambulisha kwa jina la Lucas Benedikto amesema chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo kutaka kulipita lori la mizigo katika mlima huo ambapo aliligonga lori hilo na kupinduka.





KIJANA AUAWA, ATUPWA MTO NGERENGERE

Mwili wa marehemu ukitolewa katika Mto Ngerengere eneo la daraja la Mbuyuni kata ya Kihonda mkoani hapa.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
KIJANA Moja ambaye hajafahamika jina lake wala sehemu anayoishi ameuawa kikatili na watu wasiojulikana na baadaye wauaji hao kuutupa mwili wake katika Mto Ngerengere eneo la daraja la Mbuyuni kata ya Kihonda mkoani hapa.

Akizungumza na mtandao huu, mwenyekiti wa serikali za mitaa wa Mbuyuni, Ramdhani Hamis Mpoto, alisema kwamba alipokea taarifa toka kwa wananchi wanaolima mboga mboga pembezoni mwa mto huo kwamba kulikuwa na mtu amekufa eneo hilo la daraja.

"Huyu ameuwawa maeneo ya mtaa wa Godesi na huenda wahusika wa mauaji haya walikuja kumtupa kwenye mto ili kupoteza ushahidi. Hata hivyo, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, mwili wa marehemu ulikwama katika moja ya visiki vilivyo kandoya mt. Tumebaini haya baada ya kufuatilia damu toka hapa mtoni mpaka mtaa huo wa Godesi maana njia nzima imetapakaa damu," alisema mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo pia alilaani vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi kwa kutoa roho za wenzao kwa visingizio mbalimbali vikiwemo vya wizi na ugoni

"Ni kweli inauma sana mtu kuibiwa lakini tukumbuke kwamba roho ina thamani kubwa hata kama ni mwizi au mgoni wahusika wangemfikisha kwenye vyombo vya dola husika. Mimi nalaani sana matukio haya ya kuua watu kikatili," aliongeza kusema mwenyekiti huyo.

Mara baada ya polisi kuupoa mwili wa marehemu huyo mwandishi wetu aliushuhudia ukiwa umefungwa kamba miguuni na mikononi huku sehemu ya paji la uso wake ikiwa na majeraha makubwa.

Zifuatzo ni picha za tukio hilo:

DKT. BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SONGEA LEO


DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini, Metson Mwakanyamale (kushoto) kuhusu ufugaji wa Mamba, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma, kwenye Uwanja wa Majimaji.



Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya za Songea baada ya kuwasili mjini Songea.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Moa wa Ruvuma.
Ngoma ya asili ya makaribisho ya Makamu wa Rais kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea.
Dkt. Bilal, akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa mjini Songea.

DKT. BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SONGEA LEO

Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma, kwenye Uwanja wa Majimaji.


Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya za Songea baada ya kuwasili mjini Songea.
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Moa wa Ruvuma.
Ngoma ya asili ya makaribisho ya Makamu wa Rais kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea.
Dkt. Bilal, akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa mjini Songea.