Social Icons

Wednesday, February 2, 2011

"DEMU" AICHENGUA MIDUME KWA KUKONTRO MPIRAMSICHANA mmoja, Azile Charles, mkazi wa mkoani Morogoro, jana jioni alisababisha mchezo wa robo fainali ya

MSICHANA mmoja, Azile Charles, mkazi wa mkoani Morogoro, jana jioni alisababisha mchezo wa robo fainali ya ligi ya kugombea jezi kati ya timu ya Home Boys na Terminal iliyokuwa ikipigwa Uwanja wa Saba Saba, mjini hapa, kukosa msisimko kufuatia msichana huyo kuwateka mashabiki waliofurika katika mchezo huo uliozikutanisha timu hizo zenye upinzani mkali.
Wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko, mashabiki hao walimuomba demu huyo anayefahamika zaidi kwa jina la Gaucho kuwaonyesha umahiri wake wa ‘kukontroli’ soka ambapo aliingia katikatika ya uwanja huo na kuanza kuuchezea mpira atakavyo ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo akiwa amekaa chini.

Akizungumza na mtandao huu, Gaucho (jina la mcheza soka mahiri wa Brazil, Ronaldinho Gaúcho) huyo wa ‘Mji Kasoro Bahari’ alidai ana uwezo mkubwa wa kusakata soka lakini amekosa vifaa vya kufanyia mazoezi na kukosa nafasi ya kuonekana kwa wapenda soka.
Mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo kupuliza kipenga cha kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo, uliozikutanisha Terminal inayomilikiwa na wapiga debe wa stendi kuu ya mabasi ya Msamvu na Home Boys inayomilikiwa na wauza samaki wa soko la Mji Mpya, mashabiki lukuki waliolipa kiingilio kwenye mchezo huo walisikika wakidai walivutiwa zaidi na shoo ya demu huyo kuliko mchezo huo wa robo fainali uliozikutanisha timu hizo pinzani ambapo kila timu ilionyesha jeuri ya fedha kwa kukodi wachezaji wenye majina mkubwa ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.

ZIFUATAZO NI PICHA ZA TUKIO HILO:

' KAMSEMO KA' LEO BAANA!'

Ndugu Zangu,
”UNAPOTAKA kusema, tumia yako hekima. Neno liwe la heshima. ”- Remmy Ongala.
Naam. ’Chumvi ’. Nataka kusema kuhusu chumvi. Chumvi ni maisha, chumvi ni siasa. Kwa wengine wataona ni kitu kigogo sana. Hapana, chumvi ni kitu kikubwa. Sukari na utamu wake hauzidi utamu wa chumvi. Kwanini? Maisha yaso chumvi si maisha. Ndio, maana, Serikali zote Afrika huheshimu bei za chumvi. Ukimwona raia wa nchi anaanza kulalamikia bei ya chumvi, basi, hizo si ishara njema.
Mwanadamu waweza kuwa na kila kitu nyumbani. Lakini, ukikosa chumvi nyumbani , basi, huna kitu! Chumvi ni mwandani pia, au?
Haya, umenunua nyama, vitunguu, nyanya na vingine. Jikoni unakaangiza. Kumbe! Unakumbuka, kuwa umesahau. Nyumbani huna chumvi. La haula! Giza limeshaingia, utakitafuta hata kibanda cha masikini, ukaombe chum… Shii! Usiku kuna mwiko wa chumvi. Usiku usiseme chumvi, sema ’ dawa ya mboga’. Na unajua maana yake? Wazee wetu walikuwa na busara sana. Aliyesahau kuwa na chumvi nyumbani alikumbushwa kwa kupewa ’ tabu kidogo’ katika kuipata. Maana, chumvi ni muhimu nyumbani.
Ndio, chumvi ndio dawa ya mboga. Nyama ulokaangiza haiwezi lika bila chumvi ati! Kama kuna ’ nyama ya ulimi’, basi , chumvi ndio ’ asali ya ulimi’. Na chumvi ina kawaida yake. Ikiharibika ndo basi tena, ni ya kutupwa hiyo. Chumvi haioshwi.
Na mwanadamu chunga ulimi wako. Neno lako ni chumvi. Fikiri kwanza kisha ulitamke, usitamke kisha ukafikiri. Neno baya ni sawa na chumvi iliyoharibika. Haiosheki, ikasafishika, na ikabaki kuwa chumvi.
Na mwanadamu akisemwa amekula chumvi nyingi ina maana ameishi miaka mingi. Amefaidi maisha. Binadamu aweza kupitisha siku bila kula chenye sukari. Lakini, hakuna siku ipitayo kwa mwanadamu bila mdomoni mwake kumeza kitu chenye chumvi. Na kama si chakula, basi mate, yana chumvi! Na nikisema chumvi ni tamu kuliko sukari nani abishaye?
Mh! Chumvi! Na hilo ni Neno La Leo.

CCM YASHEREHEKEA MIKA 34 YA KUZALIWA KWAKE

Baadhi ya viongozi wa CCM wakifuatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikiporomoshwa na kundi la Mwaluvistanyo ambao ni muungano wa majina matano: Mwansiti, Luiza Mbutu, Vicky Kamata, Stara Thomas na Nyota Abdallah ambaye zamani alikuwa akijulikana kwa jina la Nyota Waziri.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) jana kilizindua sherehe zake za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake miaka 34 iliyiopita. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Biafra, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Rais Mstaafu wa Zanzibar na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Visiwani, Dk. Amani Abeid Karume, ambapo pia sherehe hizo ziliambatana na utoaji vyeti vya shukhrani kwa wale waliochangia na kufanikisha chama kushinda katika uchaguzi mkuu.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Yusuph Makamba (kushoto), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa.


Khadija Kopa akitazama kwa makini jinsi Mwaluvistanyo (hawako pichani) wakishambulia jukwaa.

Dk. Amani Abeid Karume akimkabidhi mmoja wa wafadhili wakubwa wa CCCM waliofanikisha ushindi wa chama hicho, Moses Valentino Katabaro, ambaye ni Mwenyekiti wa Moses Foundation Tanzania.

Baadhi ya wasanii wa Mwaluvistanyo wakishambulia jukwaa wakiwa na msanii Dokii (katikati) ambaye aliungana nao.

Nyota Abdallah akiwa katika pozi jukwaani.

ZANTEL LAUNCHES NEW DATA SITE AT KIBETA, BUKOBA



Kagera Regional Commissioner Mohammed Babu cutting a ribbon to launch Zantel’s new site for internet connectivity in Bukoba town. Looking on is Zantel Head of PR & Events William Mpinga.

Kagera Regional Commissioner trying out Zantel’s internet after a switching on ceremony for Zantel’s data tower at Kibeta in Bukoba. Beside him is Zantel Head of PR & Events William Mpinga.



Zantel, the most trusted name in mobile broadband and internet services in the country today launched a new (data) internet site at Kibeta area in Bukoba bringing internet connectivity for the first time in the heart of Bukoba town.


Zantel Ag. Marketing Director Brian Karokola speaking at a short ceremony to switch on the new site said “Today we are here in Kibeta in Bukoba to launch this CDMA site that will bring the best internet connectivity for the first time in Bukoba town. Our data services are exceptional in terms of quality of service, affordability and network coverage.


The demand is high for internet connectivity as the world has now become a global village and as a network and service provider we are expanding our data network to meet that demand. This is a beginning as we have plans to open more sites in Bukoba and surrounding areas to ensure everybody has access to fast and reliable internet connectivity all the time.” explained Mr. Karokola.


To enjoy this once in a lifetime opportunity, Bukoba town residents simply need to visit our Zantel depot on Uganda road to purchase a modem for only TSH 49,900. With Zantel internet connectivity a customer has access to fast and reliable internet any time of the day for as low as TSH 6,000 per day.


On his part Kagera Regional Commissioner Hon. Mohammed Babu who was the guest of honour at the switching on ceremony thanked Zantel on behalf of government and Bukoba residents. “This is a big milestone for Bukoba as internet services have now come to our doorsteps as they have brought connectivity that will serve us well. As a government we support your efforts and wish you all the success as you expand your network to more towns around our region of Kagera.” said Hon. Babu.


Zantel CDMA (data/internet) network is available in over 20 regions around the country, both in the mainland and Zanzibar. “We have extensive CDMA network coverage around the country covering all the major commercial towns and cities. With the addition of this new site in Bukoba our customers are assured of access to high speed internet connectivity from the widest network in the country.” concluded Mr. Karokola.


With the coming of EASSy submarine cable that offers greater capacity internet connectivity in Tanzania is expected to increase and become more affordable for everyone. Zantel is happy to drive this positive change of bringing internet connectivity to all Tanzanians.

BONGO ACCESS YA CLOUDS TV YAZINDULIWA


Mmoja wa wakurugenzi waandamizi wa Clous Media Group,Ruge Mutaba akimpa maelekezo mafupi Dj Aron.
Mratibu wa mambo ya Live wa Clouds TV Ruben Ndege a.k.a Ncha Kali akifafanua jambo kuhusiana na hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kipindi kipya cha Clouds TV kiitwacho Bongo Access,mbele ya camera ya Clouds TV usiku wa kuamkia leo.
Msanii mahiri wa kizazi kipya,Beka Boy akiimba moja ya wimbo wake mbele ya wageni waalikwa kwenbye hafla hiyo ambayo ilirushwa Live kupitia Clouds TV.
Mdau aliyejinyakulia king'amuzi,kati ni mtangazaji wa kipindi cha Bongo Access,Ceasar.
Baadhi ya wasanii waliofika kushuhudia uzinduzi wa kipindi hicho,pichani kulia ni ,Amini kutoka THT,Ali Kiba,T.I.D pamoja na mdau mwingine.
Wageni waalikwa wakiwa wametoa pozi la picha.
Mtangazazi wa clouds FM,Dina Marios (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa taasisi ya Tanzania Mitindo House,Khadija Mwanamboka pamoja na Miss Tanzania 2010/2011 Genevieve Emmanuel wakifuatilia uzinduzi wa kipindi kipya cha Clouds TV.
Wadau mbalimbali wa mambo ya filamu pia walikuwepo kushuhudia hafla ya uzinduzi wa kipindi hicho.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo kwa makini .
Mambo ya kwaitizzz kama kawa wageni waalikwa walijimwaya mwaya vilivyo.
Kiana aina ya wageni waalikwa usiku huu hapa mjengoni Clouds Media Group.
Wageni waaliwa kwajimwa mwaya kwa raha zao yote hiyo ni mpango mzima wa Bongo Access.

Picha: Jiachie Blog.

MAPACHA 3 NA SWAAGER ZA MZALENDO PUB

Baadhi ya wanamuziki wa Mapacha 3 wakifanya makamuzi.
Khadija Shaib 'Dida wa mcho...' mbele ya Cast........
Mwanamuziki wa FM Academia Pablo Masai (kulia), akiwa na Mulemul (katikati), mwishoni ni rafiki yao ambaye jina lake sikulinyaka mara moja.
Mwanamuziki wa bendi ya FM Academia Patchou Mwamba (kushoto), akiwa na mtoto wa mjini Sadah.
Mzee wa Bandari (wa kwanza kulia), akiwa na baadhi ya wanamuziki wa Diamond Musica.
Chokora akinyoosha mbavu na kiburudisho!
mzee wa Henkein akikamua na Mapacha3

Shumileta katika pozi

MANISPAA YA ILALA YAKABIDHIWA MAGARI YA TAKA

MKURUGENZI wa Kampuni ya G.F Trucks & Equipment Ltd, Imran Karmal (kushoto), akimkabidhi mfano wa funguo, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi malori sita ya kuzolea taka kila moja likiwa na thamani ya Sh. Milioni 115 kwa Manispaa hiyo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Mehboob Karmal. Wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Jamii na Uchumi, Angela Malembeka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya G.F Trucks & Equipment Ltd, Mehboob Karmal (kulia) akimuonyesha Meya wa Manispaa ya Ilala, Jrry Slaa, Malori manne kati ya sita, yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Manispaa ya Ilala kwa ajili ya kuzolea takataka, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Meya wa Ilala, Jerri Slaa, akizungumza wakati wa hafla hiyo na wageni waarikwa.