Social Icons

Friday, January 28, 2011

MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NAIROBI

Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli (kulia) akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya (European Union) Tim CLARKE wakati alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya miradi ya barabara inayogharamiwa na Jumuiya ya Ulaya. (EU) hususani maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mandela.Picha na Hisani ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano- Wizara ya UJENZI.
Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli akiongea na Balozi wa Israel kwa nchi za Afrika Mashariki ambae ofisi yake ipo Nairobi Kenya Jacob Keidar hivi karibuni alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.Mazungumzo hayo hususani Israel kujenga nyumba nafuu nchini Tanzania kwa gharama nafuu kwa ajili ya wafanyakazi Serikalini pamoja na Taasisisi.
SHIRIKA LA NDEGE LA QATAR LAPANUA WIGO NA KUBORESHA HUDUMA ZAKE AFRIKA MASHARIKI

Safari za mara kwa mara za nchini Kenya na Tanzania na nyongeza ya safari 12 kwa wiki, kwenda Nairobi mara mbili Kwa siku, safari tano zaidi kwa Dar es Salaam.

Shirika la ndege la Qatar leo limetangaza kupanua mtandao wake wa Afrika Mashariki kwa kuongeza safari 12 zaidi kupitia miji mikuu miwili – Dar es Salaam na Nairobi.

Mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, hivi sasa una huduma kila siku, kupata nyongeza ya safari nne kwa wiki kutoka mwezi Januari. Safari za nyongeza kuanzia Februari 14 zitachukua mzunguko hadi wiki 12 za huduma.

Safari za kila siku kutoka Nairobi kwenda Doha zimeongezeka hadi kufikia safari 12 kwa wiki. Kuanzia tarehe 3 mwezi Januari safari za nyongeza mbili zitachukua nafasi hadi mara mbili kwa siku.

Safari zote zinatolewa na ndege aina ya A320 zikiwa na viti 12 vya daraja la pili na viti 132 daraja la tatu.

Bara la Afrika ni mojawapo ya soko kubwa la Shirika la ndege la Qatar kwa idadi ya vituo linavyohudumia na mji pekee kutengeneza zaidi ya asilimia10 ya mtandao wa kimataifa wa shirika hilo.

Shirika la ndege la Qatar hivi sasa linasafiri katika miji 14 Afrika, ikiwemo Alexandria, Aljeria, Misri, Luxor, Casablanca, Cape Town, Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, Dar Es Salaam, Shelisheli, Tripoli na Tunisia.

Kutoka kila mji, Shirika linatoa ofa kwa kupitia kiungo chake cha Doha kufikia vituo vingi kwenye mtandao wake Ulaya, Mashariki ya kati, Asia kusini na kaskazini pamoja na Amerika ya kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Qatar Bw. Akbar Al Baker alisema "Tunayo furaha kutambulisha upatikanaji wa safari za nyongeza kwa Afrika na kutoa ofa kubwa ya kwa abiria kuchagua ndege kutoka na kwenda kwenye miji.

“Kama sehemu ya mkakati wa ukuaji wetu, tunaendelea kupiga hatua mbele katika safari za mara kwa mara, katika vituo ambapo ni hatua madhubuti kuongeza ukuaji wetu katika nyanja za biashara na Utalii.

“Safari ya Dar es Salaam limefanya vizuri zaidi kwa kipindi cha miaka mine iliyopita ambapo ilizinduliwa mwezi Januari mwaka 2007”

“Mara kwa mara tumekuwa tukihudumia Nairobi tangu mwezi Novemba mwaka 2005 na hii imekua moja ya historia ya mafanikio makubwa Afrika, kwa hiyo tunayofuraha kuwapatia abiria wetu nafasi zaidi kwa kuongeza safari hadi kufikia mara mbili kwa siku,” aliongeza.

Zaidi ya miezi minne ijayo, ukuaji wa shirika utalenga Ulaya likiwa na vituo vipya vinne vitakavyotambulishwa– Budapest (Januari 17), Bucharest (Januari 17), Brussels (Januari 31), na Stuttgart (Machi 6), kabla ya kuzindua kituo chake cha 100 kwa mji wa Syria wa Aleppo tarehe 6 Aprili.

Hivi karibuni shirika linaendesha safari zake za ndege 93 katika vituo vikubwa vya biashara kupitia Ulaya, Mashariki ya kati, Afrika, Asia Pacific, Amerika ya kaskazini na Kusini. Kituo kipya kilichoongezwa ni Meditterrania ya Ufaransa tarehe 24 mwezi Novemba.

Kufikia mwaka 2013 Shirika la ndege Qatar linapanga kutoa huduma katika vituo 120 ulimwenguni likiwa na lengo la wastani wa ndege 120 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Ratiba ya safari mpya za Afrika Mashariki

DAR ES SALAAM - DOHA
Jumatutu, Jumatano, Alhamisi na Jumapili – kuanzia Januari 2
Kuondoka Dar Es Salaam QR547 saa 1815, kufika Doha saa2350
kuondoka Doha QR546 at 1120 saa, kufika Dar Es Salaam saa 1715

Jumamosi – kuanzia Februari 14
Kuondoka Dar Es Salaam QR547 saa 1815, kufika Doha saa 2350
Kuondoka Doha QR546 saa 1120, kufika Dar Es Salaam saa1715

NAIROBI - DOHA
Jumatatu, jumatano, Alhamis, Jumamosi na Jumapili
Kuondoka Nairobi QR535 saa 1850, kufika Doha saa 2345
KUondoka Doha QR534 saa 1230, kufika Nairobi saa 1750

Jumanne na Ijumaa – kuanzia Januari 2
Kuondoka Nairobi QR535 saa 1850, kufika Doha saa 2345
Kuondoka Doha QR534 saa 1230, kufika Nairobi saa 1750

2O% ATUNUKIWA GITAA NA PRODUCER WAKE

MWANDAAJI wa muziki, John Water (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Gitaa aina ya Aucustic lenye thamani ya Sh. 200, 000, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abas Hamis ’20%, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa msanii huyo anayeendelea kufanya vizuri katika anga za muziki wa Bongo Flava. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye Duka la City Music Sound lililopo Mtaa wa Uhuru Dar es Salaam.

Msanii huyo 20% akijaribu kupiga gitaa lake baada ya kukabidhiwa.

Picha: Sufianimafoto blog.

AIRTEL, KUKUTANISHA MAKAPUNI ZAIDI YA 40, KWENYE BONANZA LAO LA FEBRUARI 12 MWAKA HUU

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Kampuni ya Airtel Tanzania Beatrice Singano (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha la Wanahabari linalotarajiwa kufanywa na kampuni hiyo Februari 12 mwaka huu, Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Mutta Muganyizi.
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeandaa Tamasha la waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari litakalofanyika Februari 12 mwaka huu katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama, Dar es Salaam.
Hatua hii ya Airtel ni katika kutambua umuhimu wa tasnia ya habari nchini lakini pia ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa kikazi baina ya pande hizi mbili zinazotegemeana katika utendaji wao wa kila siku.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema hatua hiyo ni ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili hizo na kwamba bonanza hilo litaziwezesha pande mbili husika kufahamiana zaidi.
Alisema wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kwamba Airtel wameona ni kitendo cha uungwana kwao kuonyesha thamani waliyonayo wanahabari kwa kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo.
“Ni kawaida katika kila mwisho au mwanzoni wa mwaka kufanya tathimini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda lakini pia huwa tunakitumia kipindi hiki kukaa na kufurahi kwa pamoja na watu wenye majukumu tofauti katika kulijenga taifa ambapo miongoni mwao ni nyinyi wanahabari,” alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na burudani tofauti pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya kubahatisha ambapo wanahabari wataweza kujishindia zawadi tofauti kutoka Airtel.
Kampuni ya Capital- Plus International (CPI) ndio waratibu wa tamasha hili ambapo Mratibu Mawazo Waziri aliitaja michezo itakayohusika kuwa ni pamoja na mpira wa miguu ikihusisha timu ya watu saba kila upande, pete,kuvuta kamba na kuruka kwa magunia ambapo katika burudani kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza dansi.
Alisema taratibu nyingine kuelekea katika tamasha hilo zitaendelea kutolewa kadri siku zitakavyosonga ambapo aliahidi wanahabari kupata burudani ya kipekee katika tamasha hili la aina yake katika medani ya Habari.
“Airtel chini ya uratibu wetu imedhamiria kuwapa wanahabari burudani ya kipekee kwani mchango wenu kwao pia umekuwa wa kipekee,” alisema Waziri.

DOWANS YAWASILISHA OMBI LA USAJILI MAHAKAMA KUU

Kampuni ya Dowans leo imewasilisha rasmi maombi ya madai ya usajili wa TUZO katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa kupewa namba ya usajili nane ya mwaka huu.

Kampuni ya Dowans ilishinda kesi ya madai dhidi ya TANESCO katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kuamuliwa TANESCO kumlipa Dowans Sh Bilioni 94.

Naibu msajili mwandamizi wa mahakama hiyo Mh. Salvatory Mwongole,ameiambia Globu ya Jamii kwamba maombi hayo yameifikia mahakama hiyo januari 25 mwaka huu na yamewasilishwa na wakili wa kampuni hiyo hapa nchini kutoka kampuni ya uwakili ya Kennedy Fungamtama.

Mh. Mwongole amesema maombi hayo yamekwishapangiwa jaji lakini kulingana na unyeti wa suala hilo jina la jaji linahifadhiwa kwa sababu ndio kwanza ameteuliwa kushughulikia maombi ya usajili huo na jalada halijamfikia.

Alisema maombi hayo ya usajili yameombwa na kampuni ya Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa mujibu wa sheria TUZO hiyo haitasajiliwa hadi mahakama itoe nafasi kwa mdaiwa kuwasilisha pingamizi kupinga usajili wa Tuzo hiyo kama anaona haifai kusajiliwa, na kama hana pingamizi itasajiliwa kama imekidhi sheria na mdaiwa kulazimika kulipa fedha hizo.

Wadau wengine pia wana nafasi ya kuwasilisha maombi yao kama wanadhani usajili wa TUZO hiyo haustahili nayo pia yatapokelewa, Mahakama ikishasikiliza kama kuna mapingamizi itatoa maamuzi kama ni kuisajili au la.

REDSUN,JOH MAKINI,BELL 9 NA BEKA KUKAMUA USIKU WA VERSITY NITE NEW MAISHA CLUB

Msanii Swabri Mohamed (Redsun) kutoka nchini Kenya akifafanua jambo mapema leo asubuhi kuhusiana na shoo yao kabambe ya Versity Nite ambayo itawakutanisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu itakayofanyika leo usiku ndani ya New Club Maisha,jijini Dar.Redsun ameahidi kufanya kamuzi kubwa kwenye shoo hiyo.
Msanii wa kizazi kipya Bakari Hassan (Beka Boy) akizungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi ambaye pia atashiriki kwenye shoo ya Versity Nite itakayofanyika usiku leo ndani ya New Club Maisha,kushoto kwake ni Msanii kutoka nchini Kenya,Swabri Mohamed (Redsun) akifurahia maelezo ya Beka Boy.ukiachilia wasanii hawa,wengine ni Joh Makini pamoja Belle 9 ambao kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao hawakuweza kutoka katika mkutano huo na wanahabari.

MWANAMUZIKI WA MSONDO AFARIKI DUNIA


Malik enzi za uhai wake.
Mwanamuziki wa Bendi ya Msondo Music, Hamis Malik maarufu kama Super Malik, leo asubuhi amefia Hospitali ya Anglikan iliyopo Buguruni Malapa jijini Dar baada ya kukimbizwa hapo alipopatwa na homa kali.



Malik (kulia) akiwajibika jukwaani na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo.