Social Icons

Tuesday, August 10, 2010

BASATA

Khadija Mwanamboka akiwa na baadhi ya viongozi wenziwe walichaguliwa kuongoza Shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja anayemfuatia ni Rais wa shirikisho hilo Adrian Nyangamale, akifuatiwa na Mkurugenzi wa baraza la sanaa Tanzania Mh. Anjela Ngowi, katibu wa baraza la sanaa Ghonche Matelego mwenye shati la kijivu pamoja na katibu wa shirikisho hilo mwenye shati la maua maua pamoja na wajumbe wa shilikisho hilo.

Khadija Mwanamboka akifurahia ushindi baada ya kupata ushindi kwa kishindo .


Khadija Mwanamboka akisikiliza matokeo kwa umakini wa hali ya juu.


Mwanamitindo maarufu nchini Khadija Mwanamboka akiomba kula kwa wanachama kugombea nafasi ya umakamu wa Raisi wa shirikisho hilo.


katibu mkuu wa baraza la sanaa la Tanzania Ghonche Materego akitoa maelekezo kwa wanachama wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania {Shisuta} pembeni yake ni mkurugenzi msaidizi wa Baraza la sanaa Tanzania Mh. Anjela Ngowi.



Monday, August 9, 2010

RAHA ZA FIESTA 2010

Kila aliyehudhuria onesho la Fiesta 2010 (Jipanguse - Rraaa ) aliondoka na tabasamu kwa kukubali kwamba kilichofanyika juzi (Jumamosi) kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar haijawahi kutokea kwani ilitisha kwa matukio na burudani.

Lil Kim na Sir Nature wakifanya mambo jukwaani
Alichokifanya mwana Hip Hop wa Marekani aliyekatikiwa mshipa wa aibu, Kimberly Denise Jones ‘Lil Kim’ jukwaani na Mfalme wa Temeke, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, tukio la staa wa Clouds FM, Fatma Hassan ‘DJ Fetty’ kupigana na mengineyo ni vichache kati ya vionjo vingi vya Fiesta 2010.

Dj Fetty akizipiga na mdada
The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lina mzigo kamili, kwani lilikuwepo Leaders kuchukua sinema kamili iliyoanza Jumamosi majira saa 9 alasiri na kipimo cha kwanza kinachosherehesha kuwa Fiesta 2010 ilikuwa ‘next level’ ni umati wa kihistoria uliohudhuria shoo hiyo.

...Wengine walipoteza 'memory' kama hivi
Tathmini ya gazeti hili inatoa jibu kuwa Fiesta 2010 imevunja rekodi ya maonesho yote yaliyowahi kufanyika nchini kwa kuanzia idadi ya wahudhuriaji, aina ya jukwaa na kile ambacho kilifanywa na wasanii, hivyo kumfanya kila aliyelipia kiingilio, aondoke akiwa ametii kiu yake.

..Fegi kwa sanaa, pichani ni Malkia Ngwasuma akipuliza moshi
Gazeti hili lenye uzoefu wa kutosha katika kufanya ‘kavareji’ ya matukio ya burudani nchini, linatoa jawabu kuwa jukwaa lililotumika Fiesta 2010 ni kiwango ambacho hakijawahi kutokea Bongo.
Mbali na ukubwa, ‘matirio’ ya jukwaa hilo kuanzia uimara wake, taa na vinginevyo, ni sifa ambazo zinalitofautisha na mengine yaliyotumika nchini.

...'Hands up' kama inavyoonekana pichani
Kituko kilichotia fora ni mwanadada DJ Fetty kutwangana na ‘mdada’ mwingine ambaye anadaiwa ni mfanyakazi mwenzake.
Hata hivyo, chanzo cha warembo hao kutwangana wakati shoo ya Fiesta 2010 ilipokuwa imepamba moto hakijajulikana, lakini ‘mtiti’ wao ulikuwa si wa kitoto.

Lil Kim aliyeanza kutisha tangu miaka ya 90 akiwa na ‘lebo’ ya Bad Boy Entertainment na kuvuma kwa uhusiano wake wa kimapenzi na mwana Hip Hop, marehemu Christopher Wallace ‘Notorious BIG’, alionesha kuelewa hadhira ya Bongo inataka nini na akaipa.

...Mwanadada akidhibitiwa na baunsa
Mwanamuziki huyo mwenye sifa ya ‘uchakaramu’, alipanda jukwaani na kupagawisha kwa kiwango kikubwa lakini alipoona mashabiki wanapunguza shangwe, alimuita Juma Nature ambaye aliungana naye jukwaani.
Kupanda kwa Nature jukwaani na kupiga shoo ya pamoja na Lil Kim, ilikuwa ni mseto wa ambao haujawahi kutokea, hivyo kusababisha shangwe za kiwango cha juu.

Uhodari wa Lil Kim katika kucheza staili ya ‘Mapanga Shaa’, wepesi wa kunengua wimbo wa Nature wa ‘Mugambo’ na kadhalika, ni vitu ambavyo vilimuongezea mwanamuziki huyo alama za kushingiliwa.
Kim, alizidi ‘kuiroga’ hadhira pale alipokuwa anamkumbatia Nature mara kwa mara na kumpiga mabusu, ‘manjonjo’ ambayo yaliamsha kelele.

...hapo vipi?
Kutokana na tukio hilo, muda wote Kim akiwa jukwaani na baada ya kuteremka, mashabiki walikuwa wakipaza sauti, wakimuita mwanamuziki huyo shemeji kutokana na ‘ndoa’ aliyofunga jukwaani na Mfalme wa Temeke.

Kionjo kingine ni kivazi cha Kim ambacho muda wote kilianika kufuli lake, hivyo kuwafanya baadhi ya wenye uchu, kupiga chabo chini ya jukwaa.

Kituko kingine ni mdau wa soka, Nagari Kombo aliyefanya kituko Mei mwaka huu kwa kuingia Uwanja wa Taifa na kumkumbatia staa wa Real Madrid, Mbrazil Ricardo Kaka wakati Timu ya Soka ya Taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ ilipocheza na Brazil, kushtukiwa kwenye jaribio la kumvaa Kim.

Nagari Kombo (Staa wa Kaka) akidhibitiwa na baunsa
Nagari (Staa wa Kaka), alishtukiwa na baunsa anayeitwa Michael Mwanzamwanza wakati akiwa amekwishavuka uzio wa kwanza na kujichanganya na mapaparazi kama geresha, akitafuta njia ya kumfikia mkali huyo wa Hip Hop mwenye jinsi ya kike.
Stadi wa Hip Hop Bongo, John Simon ‘Johmakini’ alidhihirisha umwamba wake wa Kaskazini na kuonesha kuwa ‘swaga’ anazijua kwa kupiga shoo ya kiwango bora.

Wasanii wengine wa Bongo waliotisha jukwaani ni Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Wanaume Family, Witness Kaijage, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Sara Kaisi ‘Shaa’, Nassib Abdul ‘Diamond’, Kikosi cha Mizinga, Barnaba na Linah (THT).

Lil Kim akifanya vitu vyake jukwaani
Washereheshaji wa shoo, Adam Mchomvu, Hamis Mandi ‘B12’ na DJ Fetty walitoa burudani ya aina yake ambayo ilipokelewa na shangwe.
Staa wa Misifaz Camp, Abdul Sykes ‘Dully’ hakufanya vizuri jukwaani kutokana na kile ambacho kilibeba tafsiri kwamba amekuwa bonge na uzito kuongezeka.

Wakali kutoka Ivory Coast, DJ Rahmatullah na mwimbaji wa staili ya Aladji, walitegemewa wangefunika lakini ilikuwa kinyume, kwani walifunikwa na wanamuziki hata wa nyumbani.
Kundi la Brackets la Nigeria, nalo lilifanya vizuri kwa kugonga ‘mchanyato’ wa nyimbo zao za zile za Kundi la P-Square.
Kwa jumla, shoo nzima ilipangiliwa vizuri kuanzia mwanzo majira ya saa 9 alasiri (Jumamosi) hadi saa 11 alfajiri (Jumapili).

...ilikuwa ni 'Tanzania make some noise'
Rangi ilipendeza muda wote, ulinzi wa uhakika ulikuwepo ingawa mishale ya saa 8 usiku, wakati mafataki yalipopigwa kumkaribisha Kim, baadhi ya watu ambao hawajazoea hayo mambo (mashikolomageni) walikimbia huku na huko wakidhani ni hatari.
Timu ya Ijumaa Wikienda iliyofanya ‘kavareji’ Fiesta ni Sifael Paul, Richard Bukos, Musa Mateja, Aziz Hashim, Hemed Kisanda na Shakoor Jongo.

SHANGWE ZA KUJIPANGUSA KWENYE FIESTA

Haikuwa ishu kujistili Fiesta banaa..

Sister P na Swaga la Fiesta RRrrrraaaaaaaaa

Friday, August 6, 2010

WADHAMINI FIESTA WATOA VYANDARUA, RANGI HOSPITALI YA M/NYAMALA POLISI OYSTER BAY

TIMU inayosimamia mpango wa burudani wa Fiesta kutoka Clouds FM chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imetoa msaada wa vyandarua dhidi ya malaria vipatavyo 300 na rangi za kupaka majengo zenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kwa Hospitali ya Mwananyamala na kituo cha Polisi cha Oyster Bay jijini.



Afisa habari wa Kampuni ya Serengeti, Teddy Mapunda (kulia), akimkabidhi msaada wa vifaa vya usafi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Zuhura Majapa. Wengine ni baadhi ya waalikwa katika shughuli hafla hiyo.

Kamanda Mkuu wa Kanda ya Kipolisi ya Kinondoni, Elius Kalinga (kulia), akisalimiana na mmoja wa wasanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Joe Makini.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kassim Mganga (kushoto), akimvalisha kifaa cha kufanyia usafi mwanamuziki, Hamad Ally ‘Madee’.

Baadhi ya wasanii na waandishi wa habari wakielekea katika vyumba vya wagonjwa tayari kwa kuwapa pole.



Kassim Mganga akiwa ameshikilia kifaa cha usafi tayari kwa kazi hiyo.




Msanii kutoka Ghana, DJ Rama Tulah ‘Alaji’ (aliyenyoosha mkono) akipaka rangi hospital ya Mwananyamala.



Mwanamuziki wa Bongo, Angelis Faber (Enji) akifanya usafi mahali hapo.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul a.k.a Diamond (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wagonjwa katika hospital hiyo na (mwisho kulia) ni mmoja wa wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.



Msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa kwenye pozi.


Mwasiti Almasi akimnong’oneza jambo Musa Mateja.






Wednesday, August 4, 2010

BINGWA WA KUTEMBEA JUU YA KAMBA!

Kutana na kijana bingwa wa kutembea juu ya kamba na kisha kuvua na kuvaa suruali juu kwa juu bila kudondoka!


Raaaaaaa!!! Ilivyochengua CCM Kirumba Mwanza

Jana Jumapili ilikuwa ni siku ya wakazi wa Mwanza kujipangusa Raaaaaah na Fiesta 2010 kwa kushuhudia shoo kali kutoka kwa wasanii wakali wa muziki wa Bongo Flava na Hip Hop. Pichani ni kinara wa Hip Hop from Rock City, Fid Q akipelekesha mashabiki wake.

Diamond akiwaimbisha wakazi wa Mwanza wimbo wake wa Mbagala ambao umefanya vyema kwa kiasi kikubwa.


Anaitwa Bell 9,kichwa kingine katika anga ya muziki wa bongofleva kikitokea mkoani Moro,akiwarusha washabiki na wapenzi wake waliofurika ndani ya uwanja wa ccm kirumba kupitia wimbo wake wa Masogange na nyinginezo jioni ya jana.

Brazameni Dully Sykes a.k.a Mr Misifa kaiwarusha mashabiki wake.

Rrrhhaaaa zikizidi mpango mzima huwa kama hivi,chini juu,juu chiini aahh freeshh.!


Sugu Mbeya, kama Dk. Slaa Karatu

Galacha wa Hip Hop na mwanaharakati mwenye sifa ya kutokata tamaa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anafunika mkoani hapa, umati wa watu unavyomuunga mkono ni kama Katibu Mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, anavyokubalika Karatu.Sugu a.k.a Mr. II aliyejiunga na CHADEMA hivi karibuni baada ya kuombwa kufanya hivyo, aliteuliwa rasmi juzi kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho Jimbo la Mbeya Mjini na baada ya hapo, mamia ya watu hasa vijana, walimzingira ili atembee nao kwa miguu.
Vijana hao, waliizingira ofisi ya CHADEMA mkoa, wakimtaka Sugu atoke nje ili watembee naye kwa miguu kwa maelezo kwamba maelefu ya wakazi wa mkoa huu, walikuwa mitaani wakimng’oja.
Hakuna kupanda gari kaka, tunatembea wote kwa miguu. Tunataka kupeleka misukosuko mitaani. Wewe ndiye mbunge wetu,” alisikika kijana mmoja, aliyekuwa jirani zaidi na mlango wa ofisi ya chama.
Hata hivyo, jaribio hilo la vijana kutembea na Sugu mitaani, lilizimwa na Katibu wa CHADEMA mkoa, Edo Makata ambaye aliwaambia kwamba hairuhusiwi kufanya hivyo kwa sababu itaonekana chama kimeanza kampeni mapema.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbeya Mjini, John David Mwambigija, naye alikuwa kwenye wakati mgumu, alipokuwa akiwatuliza vijana hao kuelewa sheria za uchaguzi, kwani wengi wao hawakutaka kumuelewa kabisa.
Sugu, alipozungumza na gazeti hili, alisema kuwa hamasa ya wakazi wa Mbeya, inampa changamoto ya kuwatumikia kwa nguvu na kwamba hatoruhusu uozo wowote.

“Nafarijika sana kwa jinsi ninavyoungwa mkono. Ndani ya muda mfupi, nimekubalika mno kisiasa. Nitafanya nao kazi na kuwatumikia kwa nguvu zote baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mbeya Mjini. Kila kitu kuhusu kujitangaza, nasubiri muda wa kampeni,” alisema Sugu.