Social Icons

Monday, July 19, 2010

TUZO ZA ZIFF; MONALISA, KAMAU WANG’ARA

Monalisa akikabidhiwa tuzo na Martin Mhando, Mkurugenzi wa ZIFF.
USIKU wa kuamkia Jumapili iliyopita, event ya utoaji tuzo katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la ZIFF, ilichukua nafasi katika ukumbi wa Ngome Kongwe, mjini Zanzibar ambapo filamu na wasanii waliofanya vizuri walitunukiwa tuzo.

Miongoni mwa wasanii na filamu zilizong’ara, ni filamu ya Ndoto za Elibidi kutoka Nchini Kenya, iliyotungwa na Kamau wa Ndung'u na Nick_Reding ambayo ilinyakua jumla ya tuzo nne, wakati msanii Yvone Cherry Monalisa alikuwa msanii pekee wa kibongo aliyenyakua tuzo ya mwigizaji Bora.

Tuzo nyingine zilizotolewa ni pamoja na Themba (Best Feature Film-Golden Dhow), Imani (Best Feature Film –Silver Dhow), The Gift (Filamu fupi bora), Pumzi (Special Jury Prize), Motherland( Best Documentary), Ndoto za Elibidi (Verona Award), Soul Boy (SIGNIS award), A step into darkness (SIGNIS Award) na My City on fire (East African Talent Award) kutoka Uganda.

Wengine ni Shungu (Sembene Ousmane Award), The gardener and his 21 flowers (Sembene Ousmane Award), My Policy (Chairman Award), Nani (Best Tanzanian Film), wakati tuzo ya Lifetime Achievement ikienda kwa Profesa Elias Eliezer Jengo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo ambaye aliondoka na tuzo ya ZIFF Ambassador.


Kamau wa Ndung’u na Nick Reding wakifurahia tuzo waliyoipata kutokana na filamu yao ya Ndoto za Elibidi.


Mzee Chilo naye alikuwepo eneo la tukio, hapa akiwa amechill na Monalisa.


Mtunzi wa filamu ya Shungu akipokea tuzo yake.


Wanuri Kahiu kutoka Kenya tuzo baada ya filamu yake ya pumzi kuibuka kidedea.


Wasanii wa filamu wa kibongo waliohudhuria kwenye tamasha la ZIFF wakiwa jukwaani.


Mtunzi wa filamu ya Nani, Sajni Srivastava akiifurahia tuzo yake.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.


Mtunzi wa filamu ya My City on Fire, Dennis Onen akiifurahia tuzo aliyoipata.


PICHA NA HASHIM AZIZ / GPL ZANZIBAR

SHUMILETA ASHEREKEA KI STAILI BIRTH DAY YAKE!

jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa staa wa kike wa filamu za Bongo maarufu kwa jina la SHUMILETA...aliandaa kijisherehe chake pale Lamada Hotels & Apartments Ilala ambako alikusanya mashoga zake na kujilia mkeki aliokuwa amewaandalia....huku akijivunia kufikisha 27 yrs duniani..!

mkeki huo....


akimlisha shoga yake Jaque

...akimlisha shoga yake Rungi

....na yeye akijisevia....ammmh!!!

....mmmmh tamuu!!!

...akiwa na washikaji zake

..pozi la Jaque baada ya kula mkeki

waswahili husema penye mtama njiwa hawakosekani.....Victor wa Buguruni huyo!!!!


Thursday, July 15, 2010

MAUJI KWENYE BAA MCHANA KWEUPE!

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam ameauwa kwa kupigwa risasi mchana wa leo katika baa maarufu ya Angels' Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi, akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo akiwa chooni na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili kulipiza kisasi kwa kumfanyia.

Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo alipopigwa risasi na kufa papo hapo!

...sehemu ya watu waliojazana kushuhudia tukio hilo la aina yake kuwahi kutokea mitaa ya Ilala!

...jamaa wakibeba maiti ya Sadam kuingiza kwenye gari la polisi

...

...gari la mwenye baa lililovunjwa vioo na vijana hao wakati wakivamia baa hiyo


JK ZIARANI JIMBONI KWA SPIKA

Mh. Rais J.K akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki, Mh. Samuel Sitta, (aliyesimamam ) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


WANANCHI WENYE HASIRA

Kwa mara nyingine tena, kile kinachoelezwa kama 'wananchi wenye hasira, kimefanya kazi yake tena baada ya kumchoma moto wa tairi kijana aliyedhaniwa kuwa kibaka. Jamaa anaonekana kijana mmoja akimsaidia Israel kutoa roho ya kibaka huyo aliyedaiwa kutaka kuiba baiskeli kwenye nyumba ya mkazi mmoja maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam leo alfajiri. Jina la kijana huyo halikuweza kufahamika mara moja.


Kijana aliyedaiwa kuwa kibaka akiteketea kwa moto na kipigo huku akiwa amevishwa tairi.


….Kibaka akiteketea! .Dah!


PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

VITUKO VYA CHARLES BABA!

Charles Baba, mwimbaji mahiri wa Twanga Pepeta anasema anahusudu sana Tatoo na ndiyo maana mwilini mwake zimejaa kibao. moja ya tatoo hizo ni hii hapa...mwenyewe anadai ni sura ya YESU...is it?

taoo la mkono mzima

siyo kama anauza viatu vya mitumba, la hasha, hivi ni sehemu ya lundo la viatu alivyonavyo ambalo alikutwa nalo kwenye gari lake akidai anapeleka kwa SHOE SHINER...anadai kila wiki hununua kiatu kipya na kuacha cha zamani...sasa amevikumbuka!!


Tuesday, July 13, 2010

MATONYA KURUDI DAR KWA KISHINDO! -globalpublishers reports

Matonya akiwa mtaani.

Na Dunsata Shekidele,Morogoro.
OMBA omba maarufu nchini, Anthony Matonya, ambaye kwa sasa ameweka maskani katika mitaa ya Morogoro mjini, amesema kwamba yuko kwenye mchakato wa kurudi jijini Dar es salaam baada ya kuona wakazi wa mkoa huo wamemzowea sana kiasi cha kumkejeli badala ya kumsaidia.

Matonya aliyasema hayo leo asubuhi ofisini kwake barabara ya madaraka eneo la Msikiti wa Jamatini alipofanya mahojiano maalumu na mwandishi wetu juu ya mustakabali wa maisha aliyokuwa akiishi jijini Dar es salaam na yale anayoishi mkoani hapa.

"Swali zuli sana umeniuliza, ukweli maisha ya hapa Morogoro kwa sasa nayaona ni magumu, hilo linatokana na watu wengi wa hapa kiunizoea na kunipita bila kunipa chochote huku wakisema kwamba hawanisaidi kwa kuwa mimi ni maarufu nchini kuliko wao, hivyo hali hiyo ya umaarufu wa kijinga inanigharimu katika kipato changu. kwa sababu hiyo, niko kwenye mchakato wa kurejea jiji Dar es salaam, nadhani kwa sasa kumepoa kidogo tofauti na wakati ule wa serikali ya Makamba,"alisema Matonya.


Matonya akikinga kopo lake kupokea kitu kidogo kutoka kwa mpita njia

matonya akiwa kazini, huku wapita njia wakimshangaa