Social Icons

Tuesday, July 13, 2010

MWALIMU APATA AIBU YA MWAKA MBELE YA WANAFUNZI WAKE!

Mwalimu Agnes (aliyekaa) akishushuliwa na mume wa Jamila akiwa shuleni tena mbele ya wanafunzi wake wa shule ya Msingi Mchangani iliyopo Mwananyamala, jijini Dar es salaam baada ya kudaiwa kumuibia mkoba shoga yake aliyemfuata nyumbani kwake kumuuzia...ilikuwa ni aibu ambayo walimu wenzake waliamua kumchangia sh 32,000 thamani ya mkoba huo ili kuepusha soo zaidi...mkasa kamili fuatilia kwenye gazeti la Ijumaa ya wiki hii hapa hapa mtandaoni..!

Shigongo aongea na Watanzania Marekani

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameongea na Watanzania waishio nchini Marekani na kuwataka kuchangia maendeleo ya Tanzania na kuwa na mtizamo mwingine kuhusu nchi yao.

Akihutubia katika mkutano wa Diaspora 2010 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Marriot Hotel, Minneapolis nchini Marekani wiki iliyopita, Shigongo alisema mafanikio hayawezi kupatikana nchini Marekani peke yake kama ambavyo vijana wengi wanadhani, bali palipo na nia kila kitu kinawezekana mahali popote bila kujali historia ya mtu wala kiwango cha elimu alichonacho.

Aliwataka vijana walioko nje kubadilisha mtazamo wao kuhusu Tanzania kwani wengi wao wamekuwa na fikra hasi kuhusu nchi yetu na wamekata tamaa.

“Ni kweli inawezekana baadhi ya mambo yanayofanywa na watu wachache nchini yanavunja mioyo na kukatisha tamaa, lakini, je, ndiyo tuache mambo yaendelee yalivyo au tuyaweke yanapotakiwa kuwa? Ni kosa kubwa sana kuikatia tamaa nchi yetu wenyewe.

“Mungu alituweka pale (Tanzania) kwa makusudi, hivyo ni lazima kila mmoja wetu, mkubwa kwa mdogo kuhakikisha tunachangia maendeleo ya nchi yetu hata kama ni kwa kutonyamazia maovu yanayofanywa na wachache, lazima tuwe tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya vizazi vijavyo kama walivyofanya walioishi kabla yetu ambao hata majina yao hayatajwi katika historia,” alisema Shigongo.

Aidha, aliwataka vijana kufumbua macho na kuziona nafasi tele za kufanikiwa zilizopo nchini mwetu badala ya kupishana na Wachina pamoja na Wazungu uwanja wa ndege wakija kuchukua kila kitu ambacho kingewafaa Watanzania.

“Huu ndiyo wakati wa nyinyi kuja nyumbani kuchangamkia nafasi za mafanikio kabla hazijaisha, huko tunakokwenda, kama mambo hayatabadilika, itakuwa vigumu sana kwa Watanzania kufanikiwa, nafasi inazidi kuwa finyu kadri tunavyozidi kupanda juu,” alisema Shigongo huku akimtaka kila mmoja kuwa na mchango kwa maendeleo ya nchi yetu.

Alisema kufanya hivyo na huku serikali ikitimiza wajibu wake, Tanzania haitabaki ile ile miaka michache ijayo, na kwamba tufanye kazi kwa uzalendo huku tukiwafikiria watakaokuja baada yetu.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Watanzania waishio nchini Marekani (DICOTA), wawekezaji wa makampuni makubwa nchini Marekani kama vile General Mills walikuwepo kukutana na Watanzania. Viongozi wengine kutoka Tanzania waliopata nafasi ya kuzungumza ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ambaye aliwahakikishia Diaspora kuwa serikali ya Tanzania iko tayari kuwasaidia pale watakaporejea nyumbani kuchangia maendeleo yetu.

Aidha, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Harry Kitilya naye aliongelea juu ya misamaha ya kodi inayotolewa kwa Watanzania walioko nje ya nchi pale wanaporejea nyumbani na alipongezwa kwa uamuzi wake wa kukifunga kitengo cha Long Room kilichodaiwa kuwa na usumbufu mkubwa na kuwa chanzo kikubwa cha rushwa na kushuka kwa mapato ya serikali.

Mwakilishi wa CRDB Bank katika mkutano huo, alifafanua kuhusu akaunti yao ya Tanzanite na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel Ole Naiko aliongelea juu ya umuhimu wa kuwekeza nyumbani. Halikadhalika, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji, Dk. Hamis Kibola alihudhuria mkutano huo.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Ombeni Sefue na kamati nzima ya DICOTA, ikiongozwa na Dk. Lennard Tenende, ilipongezwa na wajumbe waliohudhuria mkutano huo kwa maandalizi mazuri ambapo Kampuni ya Global Publishers ilipewa tuzo kwa kazi nzuri inayoifanya katika jamii ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo.

ANTI EZEKIEL AFIWA!

Mcheza filamu wa Bongo, Aunti Ezekiel, amefiwa na wifi yake aitwaye Habiba, ambaye alikuwa ni mke wa kaka yake, Mande Ezekiel. Mazishi yamefanyika jioni hii katika makaburi ya Mtoni Kijichi ambako mtandao huu ulikutana na msanii huyo akiwa na baadhi ya shoga zake wakitoka makaburini.

Anti akipewa pole na shoga yake, Fideline Iranga

Saturday, July 3, 2010

ALICE ATWAA TAJI LA MISS KINONDONI


Mtanange wa kumsaka mrembo wa jimbo la Miss Kinondoni 2010/11 jana ulimalizika katika ukumbi wa Mlimani City ambapo mrembo aliyekuwa amevaa namba ya ushiriki 4 Alice Lushiku ndiye aliyetwaa taji hilo huku namba mbili ikinyakuliwa na Irene Hezeron na Amisuu Umari akikamilisha safu ya tatu bora kwa nafasi hiyo.



Warembo waliyokuwa wakiwania taji hilo wakiwa mbele ya watazamaji.



Mkufunzi wa warembo Joketi Mwegelo (kulia), akimpatia swali la kujibu Alice Lushiku ambalo alijibu vizuri na kumuongezea ‘point’ za ushindi.


Miss Kinondoni aliyemaliza muda wake, Lulu Abraham (kulia) akimvisha taji kwa mmliki mpya wa taji hilo, Alice baada ya kuwabwaga wenzake 10 na kutangazwa mshindi.



Wanenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ wakiwajibika stejini katika kinyang’anyiro hicho.

Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku (katikati) akiwa kwenye pozi la pamoja na warembo wenzake waliyoshika nafasi za juu (kushoto)ni Irene Hezeron aliyeshika namba mbili mwishoni kulia ni Amisuu Umari aliyeshika namba tatu.

Alice akiwa kwenye pozi baada ya kutwaa taji.

Friday, July 2, 2010

HAA! AISHA MADINDA UNAMCHEKA INTERNET!

Mnenguaji namba moja ndani ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Aisha Madinda hivi juzi kati alinaswa na kamera yetu katika viwanja vya Leaders Club akichekelea baada ya kupiga picha ya pozi na Lilian Tungaraza ‘Lilian Internet’

FAGASON NA WANAYE JUKWAANI!


Rapa maridadi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Saulo John ‘Fagason’ alisherekea hivi miaka kumi ya albam za Bendi hiyo.

EEH!BRO’ NAWE HAUVUMI LAKINI UMO!

Brother man huyu amba jina lake harikupatikana haraka hivi karibuni kamera yetu ilimnasa akijiachia na mrembo ndani ya Ukumbi wa Travertine Maomeni jijini Dar