Social Icons

Monday, October 31, 2011

KOCHA WA TIMU YA VIJANA YA MANCHESTER UNITED AANZA KUFUA VIWANGO VYA VIJANA WA AIRTEL RISING STARS BONGOKocha wa soka ya vijana kutoka Manchester United, Paul Bright akionyesha kwa vitendo namna ya kusakata kabumbu wakati wa mafunzo ya kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel Rising Stars' yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Katikati ni Graham Naftali na Samir Omary (kulia).


Mkufunzi mkuu wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel rising Stars', Billy Miller kutoka klabu ya manchester United ya Uingereza, akijadili jambo na kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Vijana ya Tanzania, Kim Poulsen, wakati wa mafunzo hayo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.




Mshiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Naomi Njeri akimtoka mshiriki mwenzake Emily Auma wakati wa mafunzo ya kliniki hiyo yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.


MKUFUNZI mkuu wa kliniki ya soka ya kimataifa ya vijana ya 'Airtel rising Stars', Billy Miller kutoka klabu ya manchester United ya Uingereza juzikati alianza rasmi zoezi la kutoa mbinu hizo kuwawezesha wachezaji kujiamini na kujifunza kutokana na makosa
. Katika siku ya kwanza wachezaji walifundishwa mbinu za kiufundi na stamina
. Wachezaji hao nyota walihudhulia na kushuudia mechi ya ligi ya ndani
Dar es Salaam, Tanzania, 31 Oktoba,2011...Kliniki ya Airtel Rising Stars imeanza rasmi Jumapili 30 Oktoba 2011, huku wakufunzi wakiwataka washiriki kuiga mbinu zinazofundishwa na kutumiwa shule za mafunzo ya soka za Manchester United.
Mafunzo hayo yanayojumuisha wachezaji 16 yatazingatia maendeleo ya kila mchezaji kwa kuzingatia vipengele vitano muhimu ambvyo vitawafanya kuwa wachezaji waliokamilika. Makocha hao kutoka Manchester United walielezea vipengele hivyo kuwa ni uwezo wa kiufundi, uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka uwanjani, kujenga mwili na saikolojia.
Akizungumzia kuhusu program ya kliniki, Kocha Mkuu wa kliniki hii kutoka shule za mafunzo ya soka za Manchester United ambaye ndiye msemaji wa kliniki hiyo - Bw. Billy Miller - alisema mpango wa Manchester United unawafanya wachezaji kuwa huru na kufanya kocha na mchezaji kuwa karibu zaidi, kufanya kazi kwa pamoja ili kutimiza malengo yao.
'Mtindo huu wa ufundishaji humfanya mchezaji ajione ni mtu muhimu na wa kipekee na kumpa hamasa ya kuwa na shahuku ya kujiendeleza zaidi, na kufanya mchezaji kuwa na ali ya kujifunza kutokana na makosa pamoja na tabia na mwenendo akiwa ndani au nje ya uwanja.' Alisema Bw. Miller.
Siku ya kwanza ya kliniki hiyo kwa wachezaji hao ililenga zaidi kwenye ufundi na jinsi ya kumkabili mpinzani wakati wa mchezo na badaye kuhudhuria mafunzo ya darasani yenye kichwa cha habari - jinsi ya kuwa mchezaji mkubwa-. Hii ilitoa fursa kwa makocha na wachezaji kuzoeana na kwa pamoja wakapitia majina ya wachezaji wakubwa duniani na sehemu zao za uchezaji ndani ya uwanja.
Kwenye upande wa ufundi wachezaji walifundishwa mbinu za kumiliki na kupasiana mpira. Wachezaji walingawanyika makundi madogo, ambayo yaliwawezesha wachezaji kupeana pasi nyingi, jinsi ya kusubiri pasi baada ya kutoa na kujijengea uwezo wa kujiamini kupokea pasi hata ukiwa kwenye mazingira magumu kutoka kwa mpinzani.
Wachezaji hao 16 walichanguliwa kutoka kwenye michuano ya Airtel Rising Stars ambayo ilichezwa kutoka kwenye ngazi ya mkoa hadi ya taifa na kuhitimishwa kwa kliniki hii ambayo imeandaliwa Gabon na Tanzania. Nchi ambazo zinashiriki kwenye kliniki hii ya Dar es Salaam ni Tanzania, Kenya, Malawi na Sierra Leone.





SALHA ISRAEL KATIKA VAZI LA UFUKWENI MISS WORLD LONDON- UINGEREZA

Miss Tanzania, 2011 Salha Israel, akiwa sambamba na washiriki wa shindano la kumsaka mrembo wa Dunia linaloendelea mjini London Uingereza.
JAN POULSEN AVUTA MASHINE 22 ZA KUIANGAMIZA WA CHAD- N'DJAMENA

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.

Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu.
Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).
Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Timu hiyo inatarajia kuingia kambini, Novemba 3, mwaka huu jijini Dar es Salaam, na pia inatarajia kuondoka nchini Novemba 9, kulelekea N'Djamena kwa ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zinatarajia kurudiana tena Novemba 15, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Powered b
PBoniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari- (TFF)

ILIVYOKUWA SIKU YA MECHI YA SIMBA NA YANGA KWA MASHABIKI UWANJANI HAPO!!!

Mashabiki wa yanga, wakiingia kwa mbwembwe uwanja wa Taifa huku wakiwa na bendera yenye picha ya mtani wao wa Jadi ambapo furaha hii ilidumu hadi mwisho wa mchezo huo baada ya mnyama Simba kuchinjiwa mbali.
Mashabiki wa Timu ya Simba, wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na maneno yanayoashiria endapo wangeifunga yanga basi kocha wa Yanga Papic angeenea katika nyumba hiyo tayari kwa mazishi jambo ambalo liliwageukia wao na kujikuta kocha wao Timbe, likimzika.

Friday, October 28, 2011

AUNT EZEKIEL ASHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE NA WATOTO YATIMA

Aunty akiwakaribisha wageni waalikwa.

Baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa wametulia.

SHEREHE ya siku ya kuzaliwa muigizaji wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel iliyofanyika Oktoba 27, mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club ilifana vilivyo.

Katika sherehe hiyo, Aunty alikula chakula cha mchana na watoto yatima 65 wanaolelewa kwenye Kituo cha Umrah Orphanage kilichopo Magomeni Mikumi jijini Dar.



Moja ya keki zilizokuwepo kwenye sherehe hiyo.


Aunty akiwasha mshumaa.


Aunty akisaidia kufungua shampeni na mmoja wa watoto hao.


Mwanamitindo ambaye pia anapiga mzigo katika shirika la Bandari nchini ‘ TPA’ naye akifungua shampeni.

Mtoto akimmiminia mwenzake shampeni.


Baadhi ya mastaa waliokuwepo viwanjani hapo wakicheza wimbo wa Moyo Wangu ulioimbwa na mwanamuziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’. Wimbo huo uliombwa na Wema Sepetu.


Mtangazaji wa Kipindi cha Take One kinachorushwa katika Runinga ya Clouds, Zamaradi Mketema akiwa katika sura mpya baada ya kuwa mjamzito.


Aunty, Sinta wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kituoni hapo.



MISS TZ SALHA ISRAEL AZIDI KUZITESA ROHO ZA WAZUNGU

Miss Tanzania 2011Salha Israel (wa saba kutoka kushoto), akiwa katika pozi la pamoja na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Dunia ninalotarajiwa kufanyika hivi karibuni London nchini Uingereza. picha hii wamepiga wakiwa ziarani, Scotland ambapo Salha amezidi kuzitesa roho za washiriki wenzake ambao wanahofia nafasi.

Thursday, October 27, 2011

AIRTEL YAKABIDHI HUNDI YA MILIONI TATU SHIMIWIAfisa Mazingira wa Airtel Tanzania, Bwana Mkama Manyama (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Mililioni tatu kwa Katibu Mkuu wa Shimiwi Ramadhani Sululu,ikiwa ni kampeni ya Airtel katika dhamira ya kushirikiana kutunza mazingira kwa kuchangia na kushiriki zoezi la kupanda miti Mkoani Tanga, wanaoshuhudia kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Shimiwi Moshi Makuka na Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde, makabidhiano hayo yamefanyika makao makuu ya Airtel Tanzania Morocco jijini Dar es Salaam.
Afisa Mazingira wa Airtel Tanzania Mkama Manyama, akiongea jambo kwenye makabidhiano hayo.
Katibu Mkuu wa Shimiwi Ramadhani Sululu (kulia), akiongea jambo mbele ya wanahabari hawapo pichani.
Bwana Sululu akitoa neno la pongezi kwa uongozi wa Airtel muda mfupi baada ya kupokea hundi hiyo.
... wakiwa katika makabidhiano hayo.

Wednesday, October 26, 2011

MZEE YUSSUF USO KWA USO NA MASHAUZI JUMAPILI HII TRAVERNTINE

KATIKA hali isiyotazamiwa na wengi, Bendi ya Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic Modern Taarab, zinatarajiwa kuvaana katika jukwaa moja Jumapili hii 30/10/2011 katika Ukumbi wa Traver tine Hotel – Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mashauzi Classic inayoongozwa na Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi imekuwa ikichukuliwa kama ndiyo bendi mkuu pinzani ya wa Jahazi tangu iundwe rasmi miezi michache iliyopita.

Isha ambaye kabla ya kuunda bendi ya Mashauzi aliitumikia Jahazi iliyo chini ya Mfalme Mzee Yusuf na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia nyimbo za “Hayanifiki” na “Ya wenzenu Midomoni”.

Kwa jinsi Isha alivyoondoka bendi ya Jahazi bila kuaga imekuwa ikiaminika miongoni mwa watu wengi kuwa yeye na Mzee Yussuf ni kama paka na panya na hivyo kupelekea onyesho hilo kuteka hisia za wapenzi lukuki wa taarab.

Isha Ramadhan amedhamiria kulitumia onyesho hilo kama sehemu rasmi ya kumuaga Mzee Yussuf na kumshukuru kwa kumjenga hadi kumfikisha hapo alipo.

Katika kunogesha zaidi onyesho hilo liliopewa jina la “Usiku wa Baba na Mwana”, Tanzania One Theatre chini ya Kapeteni Komba (Mh) imetoa jukwaa kubwa kabisa litakalowawezesha watu kushuhudia onyesho hilo bila adha yoyote.

DIVA: WABONGO WANAPENDA KULAZIMISHA PENZI


Na Erick Evarist

MSHIKA 'mic' kunako redio ya Clouds Fm, ‘Diva’ amefunguka kuwa, wabongo wengi wanapenda kulazimisha penzi hata wakati linapokuwa limekwisha.

Akichezesha taya na paparazi wa Mateja20 kwa njia ya simu hivi karibuni Diva alidai kuwa kamwe yeye huwa mapenzi hayamsumbui kwa kuwa hayajali kiivyo kama wengine yanavyowatesa alisema hata ikimtokea mpenzi wake wamezinguana basi huwa haimsumbui kiivyo.

‘‘Kwanza mimi sijawahi kuteswa na mapenzi sababu huwa siyajali na hata ikitokea tumefikia hali ya kutoelewana basi ni kuchukuwa time na maisha yanaendelea kama kawa,”

‘‘ Tatizo watu wengi huwa wanapenda kubembeleza sana wakati wanajua kabisa penzi likiisha huwa limeisha wala halihitaji kubembelezana,’’ alisema Diva.

AIRTEL RISING STARS YANUKIA

Airtel Tanzania Head of Communication Department, Beatrice Singano-Mallya, emphasizes a point as she speaks to Sports Editors from various media houses on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches. The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November. Looking on are Airtel Tanzania Public Relations Officer, Jane Matinde (left) and AON Financial Controller Deepna Shah.
Sports Editor from Global Publishers Limited, Saleh Ally, gives his contribution when over 20 Sports Editors from different media houses met and exchanged views with Airtel Tanzania officials on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches.The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November.

Sports Editors from different media houses listen attentively to Airtel Tanzania Head of Communication Department Beatrice Singano-Mallya as she speaks to them on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches. The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November.

Airtel Tanzania Head of Communication Department, Beatrice Singano-Mallya, emphasizes a point as she speaks to Sports Editors from various media houses on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches. The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November. Looking on are Airtel Tanzania Public Relations Officer, Jane Matinde (left) and AON Financial Controller Deepna Shah.
Sports Editor from Global Publishers Limited, Saleh Ally, gives his contribution when over 20 Sports Editors from different media houses met and exchanged views with Airtel Tanzania officials on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches.The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November.

Sports Editors from different media houses listen attentively to Airtel Tanzania Head of Communication Department Beatrice Singano-Mallya as she speaks to them on the forthcoming Airtel Rising Stars Football Clinic to be held at the National Stadium in Dar es Salaam under the tutelage of Manchester United coaches. The clinic involving teenager footballers from Kenya, Malawi, Sierra Leone and Tanzania is scheduled to start on 30th October and end on the 3rd of November.