STELLA MBUGE ALAMBA TAJI LA REDD'S MISS KINONDONI 2011
Miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge (katikati), akiwa kwenye pozi la pamoja na mshindi namba mbili, Husna Mauld (kushoto), na mshindi wa tatu Khamisa Hassan, muda mfupi baada ya kutwaa taji hilo. Majaji wa shindano hilo wakichakachua matokea muda mfupi kabla ya kutaja matokeo. Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper (kushoto), akiwa kwenye pozi na mshindi wa pili wa kinyang'anyiro hicho Husna Mauld, mara baada ya kumkabidhi zawadi yake. Miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge, akipokea zawadi ya tv kutoka kwa wawakirishi wa Star Times, mara baada ya kutangazwa mshindi. Msanii wa sarakasi akionyesha uwezo wake Wasanii wa filamu Bongo, Yusuf Mlela (kulia), na Jacqueline Wolper, wakibadilishana jambo ukumbini hapo. Wasanii wakiigiza miondoko ya Michael Jackson Miss Tanzania 2007, Richa Adhia, akiwa kwenye pozi na rafiki yake Msanii kutoka THT, Mataluma, akitumbuiza mahari hapo Husna akionyesha kipaji chaka wakati wa kumsaka mrembo mwenye kipaji Baadhi ya watazamaji wakishangaa moja ya shoo zilizokuwa zikitolewa Mrembo na vazi la Beach Wasanii kutoka kwenye nyumba ya kukuza viapaji (THT), wakionyesha uwezo wao Walipagawisha namna hii Warembo waliyobahatika kuingia kwenye nafasi ya tano bora wakiwa kwenye pozi la pamoja Warembo walipendeza kama unavyoona mdau Mrembo akijitambulisha na vazi lake la ubunifu Mrembo katika pozi tayari kwa kuonyesha vazi la ubunifu Mambo ya ubunifu Ishu haikuwa ndogo pande hizo Washiriki katika vazi la ubunifu Mambo yalikuwa hivi wadau Husna Mauld akionenyesha vazi la ubunifu Vazi la ubunifu lilitawala Mrembo na vazi hilo Mrembo aliyetwaa taji la nidhamu kambini Elinarda, akijitambulisha kwa mashabiki Ukumbini hapo. Mmoja wa washiriki wa kinyang'anyiro hicho akijitambulisha kwa mashabiki Warembo wakpita jukwaani kuonyesha vazi la ubunifu Vazi la ubunifu lilitawala namna hii Mshiriki akinadi vazi lake la ubunifu
MSHIRIKI wa kumsaka mrembo wa miss Kinondoni 2011, Stella Mbuge, usiku wa kuamkia leo ametwaa taji hilo baada ya kuwabwaga washiriki wenzake zaidi ya 13, waliyokuwa wakichuwana ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi huyo alijinyakulia kitita cha zaidi ya dolla 1,000 za Kimarekani na tv nchi 32 kutoka Star Times. Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Husna Mauld, ambaye alilamba kitita cha dolla 800, za kimarekani na mshindi wa tatu, Khamisa Hassan, alilamba dolla 800, za kimarekani, huku akipata na milioni moja ya za Kitanzania na taji la Balozi wa Giraffe Hotel. Katika mashindano hayo, miss aliyekuwa amevalia namba 6 Fatma Pombe, ndiye aliyenyakuwa taji la miss mwenye kipaji na alipewa zawadi ya dolla 400, za Kimarekani.
No comments:
Post a Comment